Monday, June 15, 2015

ZITTO KABWE AWAHUTUBIA WAKAZI WA MKOA WA KAGERA KWA MARA YA KWANZA LEO

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, Akifurahia mara baada ya kutua Bukoba na tayari kuwahutubia wakazi wa mji wa Bukoba leo wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mashujaa/Uhuru Platform Bukoba leo Jumatatu tarehe 15 june, 2015. Kiongozi huyu ambaye amefuatana na viongozi wenzake wa juu wa chama hicho, yuko kwenye ziara ya kukitangaza chama na sera mpya ya azimio la arusha lenye usasa. Picha na Faustine Ruta, BukobaUmati wa Watu wengi waliudhuria mkutano huo leo Jumatatu katika Uwanja wa Mashujaa mjini Bukoba
Kwa mara ya kwanza Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameteta na Wakazi wa Bukoba leo tangu ajiunge na Chama cha ACT.
Wimbo wa Taifa uliimbwa
Kulia ni msanii mkongwe wa Bongo Fleva nchini, Seleman Msindi 'Afande Sele' nae aliambatana na msafara huo mjini Bukoba.
Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Samson Mwigamba, akiwahutubia wakazi wa Mji wa Bukoba leo wakati wa mkutano wa adhara kwa mara ya kwanza mjini Bukoba leo
MSANII mkongwe wa Bongo Fleva nchini, Seleman Msindi 'Afande Sele' akiteta na Wananchi mjini Bukoba wakati wa mkutano huo wa adhara katika uwanja wa Uhuru Platform

Wananchi waliunga mkono jambo hapa!
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Anna Mghira, akiwahutubia wakazi wa mji wa Bukoba leo wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Uhuru Platform leo Jumatatu juni 15, 2015 Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Wakazi wa mji wa Bukoba wakifuatilia mkutano huo wa hadhara kwa makini
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akiongea na wakazi wa Mji wa Bukoba leo Jioni jumatatu ya juni 15, 2015
Neno likakolea!
Wakazi wa mji wa Bukoba wakifuatilia mkutano huo kwa makini
Kwa makini wakimsikiliza Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe

1 comment:

  1. Ulikuwa mkutano wa aina yake. Na Jimbo la Bukoba Mjini limempata mkombozi, ndugu Fahami Matsawili. Tunataka kurejesha heshima ya Bukoba kwa kutokomeza siasa za mazoea na fitna. We are moving from 'business as usual politics' to big results politics'.

    ReplyDelete