Friday, June 12, 2015

DKT.MAGUFULI AZIDI KUPATA WADHAMINI KATIKA MIKOA YA KILIMANJARO NA DAR ES SALAAM

Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika  mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho kutoka kwa Katibu wa CCM Wilayani  Moshi mjini Mkoani Kilimanjaro.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanachama wa CCM Mkoani Kilimanjaro waliojitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumdhamini.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akisaini kitabu cha wageni huku Katibu wa CCM wilaya ya Moshi mjini akihakiki kadi za wanachama kwa ajili ya udhamini.
 Wanachama wa CCM wakimshangilia Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli wakati alipofika kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni.
 Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa fomu ya wadhamini katika Wilaya ya Kinondoni, mkoani Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanachama wa CCM mkoani Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment