Monday, June 22, 2015

MAKAMU WAPILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AJUMUIKA KATIKAMAAZISHI YA MJUMBE WA BODI YA TUME YA UTUMISHI SERIKALINI BIBI FATMA MOH’D OTHMAN

  Marehemu Bibi Fatma Moh’d Othman Mjumbe wa Bodi ya
Utumishi Serikalini ambae pia ni Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Mkoani

Pemba aliyefariki dunia Hospitali ya Muhimbili na kuzikwa Kijijini
kwao Kiwani Mkoa wa Kusini Pemba.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akijumuika pamoja na waumini wa Dini ya Kiislamu katika kumsalia Bibi Fatma Moh’d Othman aliyefariki Da es salaam juzi na kuzikwa Kijijini kwao Kiwani Wilaya na Mkoani Pemba.

Balozi Seif pamoja na baadhi ya viongozi 
wakiwasili makaburini kwa ajili ya Mazishi ya Bibi Fatma Moh’d Othman 
hapo Kiwani Mkoa wa Kusini Pemba.

 Mwili wa Marehemu Bibi Fatma ukichukuliwa na 
 wananchi mbali mbali tayari kuupeleka makaburini mahali alipotengewa  maalum kwa kuzikwa.
 Balozi Seif akijumuika pamoja na waumini na
wananchi katika kuufukia mwili wa Marehemu Bibi Famta Moh’d Othman
katika makaburi ya familia yao hapo Kiwani.
 Maakamuj wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif 

akimpa pole Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Mwanajuma Majid ambaye ni 
Mtoto wa Marehemu Bibi Fatma hapo nyumbani kwake Mtaa wa Mfenesi 
Mazizi Mkoani.
Balozi Seif akimuaga Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pembe
Mh. Mwanajuma Majid baada ya kuipa pole familia yake kufuatia kifo

cha Mama yao Mazazi Bibi Fatma Moh’d Othman.



Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  leo amejumuika
pamoja na Wananchi pamoja na wana wa Familia katikia maazishi ya
Mjumbe wa Bodi ya Tume ya Utumishi Serikalini  Bibi Fatma Moh’d Othman
aliyezikwa kijijini kwao Jimbo la Kiwani Mkoa wa Kusini Pemba.

Marehemu Bi Fatma Mohamed  alifariki Dunia Jana katika  Hospitali ya
Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu
kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Shindikizo la Damu { Blood
Pressue }.

Balozi Seif katika mazishi hayo akitanguliwa na Mkewe Mama Asha
Suleiman Iddi  pia aliambatana na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar Mh. Ali Abdulla Ali, Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mh.
Nassor Jazira, Mwakishi wa Jimbo la Kkwahani Mh. Ali Salim Mkuu wa
Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Omar Khamis Othman pamoja na Viongozi
mbali mbali wa Serikali vyama vya siasa pamoja na Dini.

Marehemu Bibi Fatma Moh’d Othman ambae ni Mama mzazi wa Mkuu wa Mkoa
wa Kusini Pemba Mh. Mwanajuma Majid katika uhai wake alishika nyafidha mbali mbali za Kiserikali amoja na Kisiasa.



Katika utumishi wa Serikali Marehemu Bi Fatma aliwahi kuwa Mwalimu
Mkuu wa Skuli za Ngomeni na Mkoani Pemba, Afisa wa Elimu Wilaya ya
Mkoani, Mratibu wa Uendeshaji na Utumishi Elimu  Pemba  Pamoja na
Mjumbe wa Bodi ya Utumishi Serikalini wadhifa alioutumikia hadi
kufikwa na mauti.

Katika utumishi wa Kisiasa Mrehemu Bi Fatma alikuwa Mwenyekiti wa
Umoja wa Wanakwake Tanzania { UWT } Wilaya ya Mkoani, Mjumbe wa
Mkutano Mkuu wa Taifa CCM, Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi pamoja na
UWT.

Pia alikuwa Mjumbe wa Kamati tekelezaji Wilaya ya Mkoani Wazazi na
UWT, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mainduzi Mkoa kuanzia
mwaka 21 hadi 215 pamoja na Mjumbe wa  Kamati ya Siasa ya Wilaya ya
Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.

Marehemu Bibi Fatma Moh’d Othman aliyezaliwa mwaka 1950 na kufikia
umri wa miaka 65 ameacha Watoto Tisa na Wajukuu kadhaa.
Mwenyezi Muungu ailaze roho ya Marehemu Bibi Fatma Moh’d Othman
mahali pema Peponi. Amin.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment