Makatibu kata wa CCM jimbo la Isimani wakiwa wamezunguka pikipiki 16 zilizotolewa na mbunge wao Wiliam Lukuvi kwa ajili ya kuwasaidia katika shughuli za kila siku |
makatibu kata na katibu wa wilaya ya Iringa wakishangilia wakati katibu wa mkoa wa Iringa Hassan Mtenga akijaribu pikipiki hizo |
katibu wa mbunge wa jimbo la Isimani Bw Thom Malenga kushoto akimkabidhi simu 16 zilizotolewa pamoja na pikipiki 16 na mbunge Lukuvi kwa ajili ya makatibu wa CCM kata |
Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga akikabidhi simu kwa katibu kata wa CCM jimbo la Isimani |
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE wa jimbo la Isimani Bw Wiliam Lukuvi emekabidhi msaada wa pikipiki 16 zenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 22 makatibu kata wote 16 wa chama cha mapinduzi (CCM )katika jimbo hilo la Isimani wilaya ya Iringa vijijini ili kuwawezesha kufanya kazi ya chama kiufanisi zaidi .
Akikabidhi msaada huo pikipiki na simu 16 leo kwa makatibu hao wa kata kwa niaba ya mbunge Lukuvi ,katibu wa CCM mkoa wa Iringa Bw Hassan Mtenga alisema kuwa mkoa wa Iringa una zaidi ya wabunge wa watano wanaotokana na chama cha CCM ila hajapata kuona mbunge anayewajali makatibu wa chama kama alivyofanya mbunge huyo wa jimbo la Isimani na kuwa kufanya hivyo ni kuongeza ushindi wa CCM .
" katika mkoa wetu wa Iringa tunaowabunge wa CCM lakini toka wameanza mbaka wanamaliza hawajapata kutoa msaada kama huo ila Lukuvi si tu anaanza leo tuseme ni muendelezo kwa ni mara kwa mara amekuwa jirani na chama kwa kusaidia makatibu hao usafiri wa pikipiki na kuwa hii ni mara ya pili anatoa msaada huo wa pikipiki baada ya zile za awali kuchakaa"
Bw Mtenga alisema kuwa Lukuvi amekuwa ni mbunge na kiongozi wa aina yake kwani amekuwa ni msaada mkubwa zaidi ndani ya chama na hata serikalini kutokana na utendaji kazi wake na hivyo mbali ya kuwa si wakati muafaka sana ila yeye kama katibu wa CCM mkoa wa Iringa anatambua mchango mkubwa na heshima kubwa ambayo mbunge Lukuvi ameonyesha ndani ya chama na katika jimbo lake la Isimani kwa kutekeleza ilani vizuri na hivyo kuwataka makatibu hao na wana CCM jimbo la Isimani kuendelea kutoa ushirikiano kwa mbunge wao.
" Mimi ni katibu wa CCM mkoa hivyo natamka wazi kuwa mbunge Lukuvi aendelee kuwa mbunge wa jimbo la Isimani kwani ni mbunge anayetambua changamoto za watendaji wake na wananchi waliomchagua na kuzitatua na ndio jambo ambalo chama kinahitaji kwa wabunge wake kuzifanya "
Katibu wa CCM wilaya ya Iringa Bw Andrew Kashililika alisema kuwa msaada huo wa piki piki katika jimbo la Isimani ni msaada mkubwa zaidi kwani hali ya usafiri kwa makatibu wa CCM kata bila jitihada za mbunge huyo hali ya utendaji kazi kwao ingekuwa ngumu zaidi.
katibu huyo alisema ushindi ambao CCM iliupata katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa CCM kushinda zaidi ya asilimia 90n katika wilaya hiyo ya Iringa vijijini ni wazi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu CCM kitaibuka na ushindi wa kishindo zaidi .
Kwa upande wake katibu wa ofisi ya mbunge Lukuvi Bw Thom Malenga alisema kuwa ofisi ya mbunge ilipokea barua za maombi kutoka kwa makatibu hao wa CCM kata kuomba kupewa pikipiki mpya baada ya zile za awali kuchakaa na hivyo kukwamisha utendaji kazi wao .
Alisema kuwa baada ya hapo ndipo Lukuvi alipoamua kutafuta pesa kiasi cha Tsh milioni 26 kwa ajili ya kununua pikipiki hizo na kuwapa mawasiliano ya simu baada ya kuwa sehemu kubwa ya jimbo hilo kuwa na mawasiliano ya simu na kutokana na kuwa na vitendea kazi vya mawasiliano itawawezesha kufikisha taarifa kwa haraka katika makao makuu ya chama.
Hata hivyo aliwataka makatibu kata hao kujaribu kuwa waangalifu katika kutumia pikipiki hizo ili kuepuka kuwasababishia ajali kwani bila uangalifu katika matumizi upo uwezekano wa badala ya kufurahia msaada huo wakaishia kujutia majeraha yatakayotokana na wao kutokuwa makini.
Bw Zacharia Kitule katibu kata wa CCM kata ya Nyang'oro akishukuru kwa niaba ya wenzake kwa msaada huo alimpongeza mbunge Lukuvi kwa kuwamsikivu na kutimiza kila anachoahidi kwa wakati zaidi na kuwa wao kama makatibu kata wapo tayari kuendelea kutoa ushirikiano zaidi kwake ili kuona anaendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo hadi hapo atakapoamua kustaafu mwenyewe.
No comments:
Post a Comment