Friday, June 12, 2015

Makamba: Tuepuke ushabiki na kuchafuana, tutaua chama

Mh January Makamba akicheza ngoma pamoja na wanachama wa CCM wilayani Njombe waliojitokeza kumdhamini

Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Januari Makamba a ushanmewaomba wanachama wenzake wa CCM walioko Njombe kutochukulia suala la ugombea kwa ushabiki kiasi cha kuzua mtafaruku ndani ya chama, jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wake.
Makamba ameyasema hayo alipokuwa akiwashukuru wanachama wenzake waliojitokeza kumdhamini ili kupata ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
"Najua katika kipindi hiki, ambacho wanachama wengi tumejitokeza kuwania nafasi hii kila mtu ametengeneza kundi la wafuasi ambao wengi wanadhani kwamba kuwa kundi la mtu mmoja basi wewe ni adui wa kundi jingine. Hili ni kosa, sote tunania njema na nchi hii, tujenge mazxingira ya kutooneana haya baada ya kupatikana kwa mgombea mmoja kwa kuungana mkono bila kuchafua wengine", alisisitiza Makamba.
Makamba ameonya pia kuhusu kuchafuana kwa watangaza nia, wenyewe kwa wenyewe ambako kutasababisha kazi nyingine kubwa ya kuanza kumsafisha mgombea atakayesimamishwa na chama muda utakapofika.
Leo mchana Makamba anatarajiwa kupokea wadhamini mkoani Songea na baadae kuelekea Mbeya mjini ambako pia atafanya zoezi hilo.

Mh January Makamba akicheza ngoma pamoja na wanachama wa CCM wilayani Njombe waliojitokeza kumdhamini
Mh January Makamba na mkewe wakiwasili katika ofisi za CCM Mkoa wa Njombe  ambapo walipokelewa na wanachama wa CCM aliokuwa na kikundi cha ngoma
Mh January Makamba na mkewe wakisalimana na baadhi ya wanachama wa CCM katika ukumbi mdogo wa CCM mkoani Njombe.
Mh January Makamba akiwaka sahihi katika kitabu cha wageni katika ofisi za CCM mkoa wa Njombe.
Mh January Makamba akipokea fomu yenye majina ya wanachama wa CCM wa Njombe waliomdhamini kutoka kwa katibu wa CCM moa wa Njombe, ndugu Mponzi. idadi ya wanachama waliojitokeza kuweka sahihi ya kumdhamini ni 72.
Mh January Makamba akizungumza na wanachama wa CCM waliojitokeza katika Ukumbi mdogo wa CCM mkoa wa njombe. January amepata idadi ya sahihi 72 za wanachama waliojitokeza kumdhani kumwezesha kupitishwa na kupewa ridhaa ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katibu wa CCM mkoa wa Njombe akizungumza na wanaCCM wa Njombe kabla ya kumkaribisha Mh January Makamba kuzungumza na wanachama wa CCM wa Njombe. ambapo amepata idadi ya sahihi 72 za wanachama waliojitokeza kumdhani kumwezesha kupitishwa na kupewa ridhaa ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mh January Makamba akimsikiliza kwa makini katibu wa CCM mkoa wa Njombe, ngugu Mponzi walipofanya mazungumzo mafupi ofisini kwa katibu huyo. mara baada ya kupokea fomu zenye sahihi za wanachama wa CCM waliomdhamini. January amepata idadi ya sahihi 72 za wanachama waliojitokeza kumdhani kumwezesha kupitishwa na kupewa ridhaa ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment