Tuesday, June 30, 2015

Dkt MUSA MDEDE apata Baraka za kuwa mbunge wa jimbo la kalenga kutoka kwa vijana wa kikatoliki wa jimbo hilo

 Dkt  MUSA LEONARD MDEDE akitoa neno katika kongamano la vijana wa Katoliki 
 baadhi ya vijana wakimsikiza mdede katika kongamano hilo.
 baadhi ya viongozi wa vijana hao wakiwa makini kumsikiliza mdede
mdede akiingia katika ukumbi uliokuwa unafanyika sherehe

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Vijana kikatoliki waliokuwa kwenye kongamano lililofanyika katika kijiji cha ulete wamewataka wananchi wa jimbo la kalenga kuelekeza macho na masikio yao kuhakikisha wanamchagua kijana mwenzao ambaye ameonekana kuwa na uwezo wa kuwa kiongozi bora na kuwaletea maendeleo katika jimbo hilo.
Wakizungumza katika kongamano hilo vijana hao walisema kuwa hawajapata kuona kijana anayejiamini na kuonesha wazi mbinu za kulikomboa jimbo katika nyanja ya kimaendeleo.
“Jimbo la kalenga linawasomi wengi lakini jimbo hilo bado halina maendeleo ya kuridhisha licha ya kuwa na vitega uchumi vingi ambavyo vingeweza kuiongezea mapato na kukuza uchumi wa jimbo hilo,kwa mipango na mbinu ambazo mose madede amezionyesha zinatufaa kabisa wananchi wa jimbo la kalenga”. walisema vijana hao.
Lakini waliongeza kwa kuwataka vijana na wananchi wa jimbo la kalenga  kutofanya makosa katika uchaguzi wa mwaka huu kwa kumchagua kiongozi anayewafaa na kujiamini kwa kuwaletea maendeleo na kuwatetea wananchi wake.
Nao viongozi wa vikalia tosamaganga walimsifu kijina moses kwa kujiamina na kuwaonyenyesha vijana wenzao kwa maneno na ujumbe wa kuwapa njia muhimu za kufikia malengo yao katika maisha.
Waliongeza kwa kusema kuwa baadhi ya vijana waliokosa hutuba ya moses mdede wamekosa kitu cha muhimu sana lakini akawaomba vijana hao wakirudi nyumbani kwao basi wafikishe ujumbe kwa wananchi na vijana waliokosa kongamano hilo kwa kuwa wao ndio mabadiliko ya sasa.
“Vijana mbadilike msiwe kama vijana wa zamani nchi hii inahitaji viongozi wenye weledi wa kuwaongoza wananchi na kuwalete maendeleo  mdede anafaa na anasifa zote za kuwa kiongozi kwa kuwa anasifa zote za kuwaongoza wanachi wa jimbo la kalenga hivyo wananchi msifanye makosa”.walisema  viongozi hao.
Kwa upande wake sister kiliana sanga wa ulete alisema kuwa hajawahi kukutana na kijana mwenye uwezo mkubwa wa kifikra na mipango madhubuti ya kuleta maendeleo ya jimbo la kalenga.
Naye moses mdede aliwataka vijana kujitambua na kushemu maamuzi yao wakati wananfanya kitu sahihi kwa wakati sahihi kuwataka wasikubali kuchaguliwa kiongozi katika uchaguzi wa mwaka huu.
“Sasa ifike wakati vijana muwe na maamuzi ya kujichagulia viongozi sahihi vijana ni taifa la leo sio la kesho hivyo ukimchagua kiongozi kwa kununuliwa ujue kuwa atakapo ingia madarakani atawaongoza anavyowataka yeye na sio kuwaletea maendeleo kwa kuwa ameingia madarakani kwa kuwanunua”.alisema mdede
mdede aliwataka vijana kuacha kulalamika kila wakati na badala yake wafanye kazi kwa kujituma ili wajiletee maendeleo na kuacha tabia ya kufaata mkumbo katika kutafuta maisha bora.
“Viongozi wa dini  nyie mnaka mara kwa mara na waumini wenu hiyo mnapaswa kuwapa elimu ya maisha na kuwajua viongozi wazuri kwa kuwa nyie mnakaramu hiyo,mfano leo hii mmekaa na vijana hao na kuwapa mafunzo mbalimbali hivyo mnapaswa kuwaambia ukweli juu ya mstakabadhi wa serikali yetu ambayo imepoteza matumaini”.alisema mdede.
Lakini  MDEDE aliwataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kuinua uchumi wa nchi.
MDEDE aliyasema katika kongamano la vijana wa katoliki katika kata ya ulete Iringa vijijini ambapo amewataka vijana kutambua umuhimu wao katika jamii ili kuleta madadiliko chanya kwa taifa.
Aidha Dkt MUSA amesema kuwa wazee ni hazina kwa taifa kwa ushauri wa mambo mbali mbali ya kiuongozi   lakini nguvu ya vijana inahitajika ili kulikwamua taifa kutoka hapa lilipo na kusonga mbele.

Monday, June 29, 2015

LOWASSA AHITIMISHA ZIARA YA KUTAFUTA WANACCM WA KUMDHAMINI MKOANI MOROGORO LEO, ADHAMINIWA NA WANACCM 104,038

Sehemu ya WanaCCM na wakazi wa Mji wa Morogoro, wakiwa wamekusanyika nje ya Ofisi za CCM Mkoa huo, kumlaki Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, pindi alipowasili kwenye ofisi hizo kukabidhiwa orodha ya majina ya WanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amehitimisha zoezi hilo la kutafura Wadhamini, leo Juni 29, 2015 katika Mkoa wa Morogoro na amedhaminiwa na WanaCCM 104,038.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma, pindi alipowasili kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Morogoro, leo Juni 29, 2015 kwa ajili ya kukabidhiwa orodha ya majina ya WanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalageris. Mh. Lowassa amehitimisha zoezi hilo la kutafura Wadhamini, leo Juni 29, 2015 katika Mkoa wa Morogoro na amedhaminiwa na WanaCCM 104,038. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Mapokezi ya Mh. Lowassa Mkoani Morogoro.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisaini kitabu cha wageni kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Morogoro, leo Juni 29, 2015. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalageris na kushoto ni Mke wa Mh. Lowassa, Mama Regina Lowassa. Mh. Lowassa amehitimisha zoezi hilo la kutafura Wadhamini, leo Juni 29, 2015 katika Mkoa wa Morogoro na amedhaminiwa na WanaCCM 104,038.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwapungia WanaCCM wa Mkoa wa Morogoro wakati alipowasili tayari kwa kukabidhiwa orodha ya majina ya WanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amehitimisha zoezi hilo la kutafura Wadhamini, leo Juni 29, 2015 katika Mkoa wa Morogoro na amedhaminiwa na WanaCCM 104,038.
Umati wa WanaCCM wa Mkoa wa Morogoro ukiwa umefurika kwa wingi wake kwenye viwanja vya CCM Mkoa wa Morogoro, kumsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa.
WanaCCM wa Mkoa wa Morogoro wakifatilia kwa makini.
Mzee Steven Mashishanga akiyarudi magoma kabla ya kupanda jukwaani kuzungumza machache na kuwasalimia WanaCCM wa Mkoa wa Morogoro.
Mzee Steven Mashishanga akizungumza machache na kuwasalimia WanaCCM wa Mkoa wa Morogoro.
Dkt. Juma Ngasongwa akitoa neno.
Mh. Lowassa akipena mkono na Dkt. Juma Ngasongwa. 
Askofu Mamio akisalimia.

Wadau Mkutanoni.
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM kutoka Zanzibar, Mzee BoraAfya akitoa salamu zake kwa WanaCCM wa Mkoa wa Morogoro waliokuwa wamekusanyika kwenye Uwanja wa CCM Mkoa huo, leo Juni 29, 2015.
Mzee Msindai katika ubora wake.
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akiwasalimia WanaCCM wa Mkoa wa Morogoro,  leo Juni 29, 2015.


Taswira mbalimbali za WanaCCM wa Mji wa Morogoro Mjini na maeneo ya jirani katika zoezi la kupokea orodha ya majini ya WanaCCM waliomdamini Mh. Edward Lowassa.
Wapiga picha wakitafuta taswira zilizo bora kabisa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akifatilia kwa makini taarifa ya Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Kulwa Mironge wakati akitaja idadi ya WanaCCM waliomdhamini. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalageris.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam, Salum Madenge akisalimia wanaCCM wa Mkoa wa Morogoro.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akifurahia jambo.

Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akifurahia jambo.
 Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Kanali Mstaafu Isack Mwisongo akizungumza jambo na kutoa historia kidgo ya Chama cha Mapinduzi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalageris akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, kutoa shukrani zake kwa wanaCCM waliomdhamini.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipokea orodha ya majina ya WanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015, kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Kulwa Mironge, leo Juni 29, 2015. Mh. Lowassa amehitimisha zoezi hilo la kutafura Wadhamini, leo Juni 29, 2015 katika Mkoa wa Morogoro na amedhaminiwa na WanaCCM 104,038.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akionyesha fomu yenye orodha ya majina ya wanaCCM waliomdhamini, kwa kadamnasi iliyokuwepo kwenye Uwanja wa CCM Mkoa wa Morogoro, leo Juni 29, 2015, baada ya kukabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Kulwa Mironge.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza machache na kutoa shukrani kwa WanaCCM waliomdhanini ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.