Hata mimi nimechukua fomu ya Urais :Naibu meya wa Manispaa ya Iringa ambae ni diwani wa kata
ya Ilala Bw Gervas Ndaki akifurahia kushika mkoba wenye fomu ya CCM
ya kuomba kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ,fomu ya Monica Mbega baada ya mgombea huyo kufika mjini
Iringa kusaka wadhamini 30
Na Matukiodaima Blog
WAKATI mbio za
makada wa chama cha mapinduzi (CCM) waliotia nia ya kuomba
kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi za urais zikiendelea kushika kasi
kwa kila mgombea kutumia mbinu yake ya kuwafikia wana CCM kuomba
udhamini , aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini Monica Mbega leo
ameingia wilaya ya Iringa mjini mkoani hapa kuomba udhamini na kupata
wajumbe 33 huku akiwataka watanzania kutoaminishwa na mbwembwe za
watia nia wenzake wanazofanya mikoani na kuwa yeye ndie Rais wa awamu
ya tano baada ya Dr Jakaya Kikwete na kuwataka watia nia wenzake
wamuunge mkono.
Mbega
ambae alilazimika kusubiri wajumbe 30 wa kumdhamni kwa zaidi ya
masaa manne katika ofisi ya CCM wilaya ya Iringa mjini alitoa kauli
hiyo wakati akizungumza na wanahabari juu ya safari yake hiyo ya
kutaka kwenda Ikulu na kudai kuwa amelazimika kuzuia viongozi wa
CCM wilaya ya Iringa kutomuandalia mbwembwe zozote wala wapambe wa
kumshangilia wakati wa safari yake hiyo ya kutafuta wadhamini.
Alisema
kuwa kuwa anamtegemea Mungu zaidi katika safari yake hiyo ya kwenda
Ikulu na ndio maana hakupenda kuweka makisio ya gharama za safari
nzima ya mchakato huo wa kuelekea kupokea kijiti kwa Rais Dr Kikwete
na hivyo ndio sababu ya yeye kuzunguka bila ya mpambe zaidi ya
dereva anayemuendesha pekee.
"
Naomba niwaelezeni wazi kuwa sina mgombea wa kumuunga mkono kati
ya wote waliojitokeza zaidi ya 30 kwani naamini kuwa namba moja
kati ya wote hao waliojitokeza ni Monica Ngenzi Mbega ninasema
hivyo kwa kuwa nchi ya sasa inahitaji mwamanke kuongoza kwani
mwenye kuweza kuvunja makundi ni mwanamke sio mwanaume tena
.....mwanamke ni mwepesi wa kusamehe sio mtu wa makundi hivyo kama
hivyo ndivyo ukitanguliza upendo makundi hayatakuwepo ila wapo wenye
visasi vya kutoka mwaka 2005 ila sio mimi ....mimi nimetanguliza
upendo zaidi....mimi ni mama nitaiunganisha nchi na changamoto
inayomkabili Rais wa awamu ya tano ni jinsi na kuiunganisha nchi na
mimi ndie pekee wa kuunganisha nchi hii"
Alisema
kuwa iwapo watanzania wataunganishwa kuwa wamoja kuna uwezekano
wa nchi kuachana na utegemezi na hivyo wananchi wake kuwa wamoja na
kuweza kushiriki kujiletea maendeleo yao chini ya rais wao Mbega .
Hivyo
alisema kuwa iwapo chama chake kitamteua na watanzania
wakamchagua na kuingia Ikulu wategemee Tanzania mpya yenye amani
,upendo na mshikamano na uchumi bora kwa kila mtanzania kuongeza
pato binafsi .
Mbega
alisema kuwa tayari Rais wa nchi Dr Kikwete amepata kuueleza
umma kuwa misaada ambayo nchi inapata kutoka kwa wahisani mingine
ina masharti magumu na ndio maana ya baadhi ya miradi kushindwa
kukamilika kwa wakati na kuwa iwapo yeye ataingia Ikulu atajaribu
kukwepa misaada hiyo na kulijenga Taifa linalojitegemea lenyewe ili
kuto kuwa na miradi isiyo kamilika kutokana na masharti magumu ya
wahisani .
Alisema
kuwa kikubwa kilichomsukuma kuchukua fomu ya kutia nia kuomba
kuteuliwa kuwania Urais ni uzalendo wake katika Taifa wenye shauku
la kuliongoza Taifa la Tanzania kama mwanamke wa kwanza toka nchi
ipate uhuru wake mwaka 1961 bila ya kuongozwa na mwanamke na kudai
kuwa hakuna mgombea wa CCM ambae anajambo lake binafsi la kufanya
zaidi ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.
"Falsafa
yangu ni kusahihisha changamoto zinazoonekana katika kutekeleza
ilani hatujaweza kufanikiwa hili ....mheshimiwa Rais Dr Kikwete
tunaona jinsi anavyotekeleza ilani katika sekta mbali mbali ila
utasikia katika vikao vya kamati kuu wakati akitoa taarifa ya
utekelezaji kuwa kuna changamoto mbali mbali ambazo zimekwamisha
utekelezaji wa ilani hivyo mimi nitaanzia kutekeleza changamoto kwanza
.....kwani bajeti inayotengwa ndio inapaswa kusimamiwa kwanza
mwelekeo mzima wa serikali yangu ni kuona tunapata Taifa la watu
wanaojitegemea wenyewe"
Katika
hatua nyingine Mbega ambae aliangushwa nafasi ya ubunge mwaka 2010 na
mbunge Peter Msigwa (Chadema) alisema kuwa bado ana nguvu ya
kurudi kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini na kumshinda mbunge wa
sasa mchungaji Msigwa kwani bado nguvu za kurejesha jimbo hilo CCM
anazo japo hana mpango wa ubunge zaidi ya kutimiza dhamira yake ya
kuingia Ikulu kama Rais aliyokuwa nayo toka mwaka 2005 na alishindwa
kuingia mwaka 2010 kwa kumheshimu Rais Dr Kikwete pekee ila sasa ni
zamu yake .
Pia
alisema CCM bado ina nguvu zaidi katika jimbo la Iringa mjini na
Tanzania kwa ujumla na iwapo suala la upendo likawatangulia watia nia
wote pale wanapokosa kuteuliwa kuungana kwa upendo kumuunga mkono
aliyeteuliwa kamwe suala la wapinzani kushinda litabaki kuwa ni
ndoto.
Wakati huo huo huo mgombea huyo
amewaacha hoi wanahabari waliofika kumsikiliza baada ya kudai kuwa
waandike majina yao kamili na namba zao za simu ili kuja
kuwakumbuka katika ufalme wake pindi atakapoingia Ikulu
|
No comments:
Post a Comment