Ndugu wanahabari leo tarehe 21 Juni 2015 nimekuiteni kuwaeleza juu ya Nia yangu ya kugombea Ubunge Iringa Mjini kwa ticket ya CCM.
Sababu ninayo Nia ninayo na uwezo ninao kwa wananchi wangu wa Iringa na Tanzania kwa ujumla.
Natambua ya kua uongoZi ni Mzigo... Uongozi ni kipaji na uongoZi ni kubeba Majukumu ya kuwaongoza wengine na siyo Ubwana au Ubwanyenye Kama dhana hii inavyoharibiwa na wengi.
Ndugu wana Habari Uongozi ni Wito... Mimi nimezaliwa hospitali ya serikali ya Mkoa Iringa na kukulia Frelimo kata ya Mivinjeni na nimekua Kiongozi tangu nikiwa Mtoto pale Sokoni Iringa Kanisa Kuu na baadae kuwa Kiranja Prefect nikiwa Wilolesi Shule ya Msingi Hali hiyo iliendelea nikawa Waziri Katika wizara mbali mbali miaka yote mitatu nilipokua Chuo Kikuu baada ya Kumaliza Masomo yangu ya Sheria CCM makao Makuu walinileta Iringa Kama Katibu wa Wilaya kazi ambayo nayo ilininoa vilivyo.
Ndugu wana Habari kazi hiyo haikuishia hapo... Katika kujifunza uongozi Mungu amenibariki kuwa Msaidizi wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Kama Mzee Makamba, George Mkuchika na Jaka Mwambi Mpaka baadae Mwenyekiti wa Chama Changu CCM aliporidhia kuanzishwa kwa taasisi ya wasomi yaani vyuo Vikuu ambapo nilipelekwa kuongoza na nikiwa huko niliweza kujenga takribani matawi yote ya vyuo Vikuu Nchi nzima kwa kuhakikisha wana kuwa na Uongozi na ofisi zao ushahidi ni hapa kwetu Iringa nilifungua matawi matatu na kujenga ofisi za Mkwawa na Tumaini.
Nimepitia mafunzo mbali mbali ya Chama tangu mwaka 2006 Katika Chuo Kikuu cha CCM Ihemi na kufaulu kwa distinction jambo ambalo linanipa unyenyekevu kuwatumikia Wananchi wangu wa Iringa.
Ndugu wana Habari nimejiunga na CCM tar 31.12.1998 Tawi la Tandamti Frelimo kwa Balozi wangu Mzee Mlosi (Mungu amuweke mahala pema) hivyo ni karibu miaka 14 nipo ndani ya Chama Changu na ninaona ninayo haki na wajibu kuwaongoza wana Iringa wenzangu ambao najua changamoto zao zinazowakabili Katika Chama na Nje ya Chama.
Ndugu wanahabari kwa kutumia uzoefu nilionao hapo juu vilevile Kama Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Rais wa WanamuZiki wa Injili Tanzania, Wakili (Advocate) na kada wa CCM Mume wa Mke Mmoja na watoto watatu, hii Kabisa ni ishara kubwa kuwa ninao uwezo wa kupambana na changamoto za Iringa Mjini na Nchi yangu kwa Ujumla.
Changamoto tuliZonazo... Ndani ya Chama...., bila kupepesa maneno natambua mpasuko uliopo na ambao umesababishwa na Viongozi wa juu wa Chama Wilayani na Mkoani hapa na wengine wamepewa nafasi za serikali lakini bado wamekipasua Chama kwa makundi hivyo mtu Pekee atakayeleta Umoja na mshikamano ni Mimi Addo November Mwasongwe ambaye sina kundi na nipo Tayari kuongoza watu wote, mtu wa watu Mpenda watu ambaye Nafahamu taratibu za Chama Changu ndio maana Mpaka leo sijafanya vurugu yeyote jimboni Kama wanavyofanya wenzangu ambao mnawajua..na mmewaona wakijipitisha kila kukicha. Mara Zote napata sana Faraja ninapokumbuka Kauli inayosema Kizuri Chajiuza Kibaya Chajitembeza Natambua changamoto ya ofisi bora za CCM na usafiri kwa kila Kata na Hilo nitalichukua Kama jukumu langu binafsi Kama mjumbe wa Kamati ya Siasa pale mtakaponipa ridhaa ya Ubunge.
Natambua kuwa mafunzo ya uongozi tanatakiwa kuanzia ngazi za shina Mpaka Kata na Wilaya.Changamoto za Wananchi
1.Miundo Mbinu na Umeme jambo hili litakua kipaumbele kuhakikisha maeneo yote yanafikika kwa Lami hii inaweZekana kwa kupata Mbunge safi ambae ni mie na madiwani safi,
2. Iringa kuwa kitovu cha Utalii Kama ilivyo Arusha... Wote tunatambua kuwa Mbuga ya Ruaha ndiyo kubwa kuliko Zote Duniani hivyo ni jukumu letu kuitangaza na kuweka vivutio vya utalii Kama vile Mahoteli makubwa Tour Guide Offices jambo ambalo litakuza uchumi wa Iringa kwa kupitia Utalii na kutoa ajira kwa wana Iringa na wengine wengi.
3. Kuwamilikisha wananchi wetu ardhi zao ili wasiweze kudhurumiwa lakini waweze kukopea inapobidi kwa maendeleo Yao
4. Kukuza Michezo na Sanaa kuwa na uwekezaji wenye tija wa Sanaa na Michezo jambo litakalotoa ajira ya kudumu na kukuza uchumi wetu,
5. Matibabu ya uhakika kwa wazee wanawake na wasiojiweza 6. Utawala bora na uwajibikaji
7. Wananchi kupata mikopo nafuu ya Nyumba
8. Kupiga Vita ukimwi na malaria
9. Kuku za Kilimo na kutafuta Masoko ya uhakika ya maZao yetu
10. Kukuza Elimu na kutoa Motisha kwa Vijana wetu walioko kuanzia Shule za Msingi na Sekondari ili tujipatie vijana wenye uwezo mkubwa kwa maendeleo ya Taifa na hili halitawezekana bila walimu bora wanaolipwa vizuri
11. Uongozi wa Vitendo
12. Kukuza Miundo Mbinu hasa usafiri wa Anga kwa kurekebisha Airport yetu ili kuharakisha maendeleo na Utalii.
13. Rasilimali ziwanufaishe wananchi wetu
14. Kukemea Rushwa na Ufisadi ifikie hatua ikibidi tuapishwe kwa Jina la Mwenyezi Mungu kuwa Kati ya Sisi Wagombea yeyote anayetumia pesa kuhonga Katika uchaguzi huu basi na afe kwa Jina la Mwenyezi Mungu kwenye hili tusilete mzaha tujiulize hawa wanaotumia pesa watazirudishaje?? Kwa Njia ipi
15. Wanawake, wazee Vijana na Watoto kuwa na Mfuko wao maalum wa kuwakwamua
16. Lugha ya Kiswahili kuitumia kama mtaji kwa kuanzisha madarasa yatakayowaleta watalii kuja kujifunza Kiswahili na ikibidi watu wetu kwenda Nje ya Nchi kufundisha Kiswahili jambo litakalonipa sana Faraja
17. Kuziba pengo Kati ya asiye Nacho na mwenye nacho.
18. Kupunguza Kabisa kero ya Maji na gharama ya maji mwananchi wa kawaida apate maji pasipo Shaka
19. Kuwa na usafiri wa Ambulance ikibidi kila Kata ili kunusuru maisha hasa Akina Mama wanaokwenda kujifungua Hospitali.
20. Kukaribisha wawekezaji wenye tija kwa maendeleo ya wote.
Ndugu zanguni ninayo mengi mema kwa Jimbo langu na Taifa langu na Ni matumaini yangu ya kuiona Iringa kwa jicho la Mwenyezi Mungu yaani Iringa ambayo Mungu anataka Iwe Kama alivyoikusudia na Kila Mmoja aweze kuridhika nayo.
Inawezekana Kila Mmoja Akitimiza wajibu wake, Mjenga Nchi ni Mwananchi. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Iringa, Mungu akiwa Upande Wetu Ni Nani aliye juu yetu??? Tujipe moyo Tutashinda Pamoja.
Addo November Mwasongwe, Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Wakili na Kada wa CCM 0754/0713396367 P.O.BOX 1215 Iringa Tanzania.
No comments:
Post a Comment