Tuesday, June 16, 2015

MTWARA WAJITOKEZA KWA WINGI KUMDHAMNINI DKT. MAGUFULI

Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mtwara.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akimsalimia mzee mwenye umri wa miaka 85 aliyejitokeza kumdhamini Mkoani Mtwara katika mchakato wa kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea Urais kutoka chama cha Mapinduzi CCM.
Mchakato wa udhamini ukiendelea kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Mtwara mjini.
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.
CCM Oyeee…Ndivyo wanachama wa CCM Wilayani Masasi walivyokuwa wakisikika mara baada ya kumdhamini Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katika Mchakato wa Kuwania nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais kupitia CCM.
wanachama wa CCM Wilayani Masasi wakimsalimia Dkt. Magufuli
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Masasi.

No comments:

Post a Comment