Saturday, December 31, 2016

KAIMU KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA AWAASA MAOFISA MAGEREZA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA UFANISI

Na Lucas Mboje, Dar es Saam
KAIMU Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa (pichani) amewaasa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza  nchini kuzingatia  kuwa utendaji wao wa kazi za kila siku uende sambamba na kasi ya Serikali ya Awamu ya tano ili kuleta ufanisi unaotarajiwa.

KAIMU Kamishna Jenerali, Dkt. Malewa ameyasema hayo jana wakati wa Baraza la Kufunga Mwaka 2016 na kuukaribisha Mwaka 2017 lililowahusisha baadhi ya Maafisa na Askari kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani pamoja na Magereza ya Mkoa wa D'Salaam.

Aidha, amewataka Maofisa na Askari wa Jeshi hilo kudumisha nidhamu wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kazi  ikiwemo kutekeleza mara moja Amri mbalimbali zinazotolewa na Viongozi wao wa Jeshi.
"Kila mmoja wenu atimize wajibu wake katika eneo lake la kazi kwa bidii, ari na moyo wa kujituma ili kuliwezesha Jeshi letu kupata ufanisi unaotarajiwa". Alisisitiza Kaimu Jenerali Dkt. Malewa.

Wakati huo huo Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa  pia ametumia fursa hiyo kuelezea baadhi ya mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kwa Mwaka uliopita 2016 ambapo Jeshi la Magereza limeweza kupata jumla ya leseni 102 za uchimbaji wa madini ya ujenzi kama vile chokaa, mawe, kokoto, mchanga na Murram katika maeneo mbalimbali ya magereza. Pia katika mwaka 2016 Jeshi limeweza kujenga nyumba 129 kwa njia ya kujitolea ambapo nyumba 231 zipo katika hatua mbalimbali ya ukamilishaji. 

Aidha, Ujenzi wa nyumba 320 za makazi ya askari katika eneo la Gereza Ukonga maandalizi ya ujenzi yanaendelea na ujenzi wa nyumba hizo ni kufuatia ziara ya Rais Magufuli  Novemba 29 mwaka huu  ambapo alipokea taarifa ya uhaba wa nyumba za kuishi askari wa jeshi hilo na akaagiza Jeshi la Magereza lipatiwe Tsh. bilioni 10 haraka ili kupunguza tatizo hilo.
Shirika la Magereza na Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa PPF wameingia Makubaliano ya Mkataba wa ubia katika mradi wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha kusakata ngozi pamoja na uwekezaji wa mashine za kisasa za kutengnezea bidhaa za ngozi katika Kiwanda cha Viatu cha Gereza Karanga, Moshi.

Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga kimepata Ithibati na hivyo kuwa na hadhi ya kuwa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji na mapema mwakani kinatarajia kudahili wanafunzi 30 katika fani ya Taaluma ya Urekebishaji ngazi ya cheti.  
Pamoja na Mafanikio hayo, Kaimu Kamishna Jenerali Dkt. Malewa ameelezea changamoto mbalimbali zinazolikabili Jeshi hilo ikiwemo ufinyu wa bajeti, makazi duni ya maofisa na askari, uhaba wa vitendea kazi, ukosefu wa pembejeo pamoja na madeni ya wabuni na watumishi wa jeshi hilo. 
Kuhusu maeneo yatakayopewa kipaumbele kwa Mwaka mpya 2017 ni kuwa Jeshi la Magereza litaendeleza jitihada za kuimarisha na kuongeza uzalishaji kwenye miradi ya uzalishaji wa mazao ya Kilimo na mifugo lengo ikiwa ni kujitosheleza kwenye chakula cha wafungwa, kuhakikisha wafungwa wanafanya kazi za uzalishaji mali kwa kiwango chenye tija badala ya kukaa tu magerezani pia kuendeleza mikakati ya kupunguza msongamano magerezani.
Baraza la kufunga Mwaka na kuukaribisha Mwaka unaofuata ni utamaduni wa siku nyingi ambao unaenziwa na Viongozi Wakuu wa Jeshi la Magereza ambapo Baraza la aina hii hufanyika kila Mwaka ili Kamishna Jenerali wa Magereza nchini aweze kuongea na Watumishi wote wa Jeshi la Magereza nchini kupitia Baraza hilo lengo ikiwa ni kufanya tathmini ya yale yaliyojiri katika Jeshi kwa kipindi cha Mwaka unaisha kwa kuzungumzia mafanikio na changamoto zilizojitokeza na  kutazama matarajio ya Mwaka mpya.

Monday, March 21, 2016

PPF KANDA YA ZIWA IMEWAFIKISHA WAAJIRI SABA MAHAKAMANI KWASHINDWA KULETA MCHANGOYAO.

MENEJA MFUKO WA HIFADHI ZA JAMII PPF KANDA YA ZIWA, MESHACK BANDAWE, AMEWAFIKISHA MAHAMANI WAAJIRI SABA KWAKUSHINDWA KULETA MICHANGO YA WATUMISHIWAO.

AKIONGEA KATIKA SEMINA HIYO NA WAAJIRI WATAASISI MBALIMBALI JIJINI MWANZA BW.MESHACK BANDAWE,FAIDA ZINAZOTOLEWA NA MFUKO WA HIFADHI ZA JAMII KANDA YA ZIWA ALISEMA MFUKO WA HIFADHI ZA JAMII UMEFANIKIWA KUKUSANYA ZAIDI YA BILIONI TISA.AMBAPO PIA WAMEFANIKIWA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WAAJIRI SABA WALIOSHINDWA KUWAKILISHA MICHANGO YAO YA ZAIDI MILIONI 500.

KATIKA SEMINA HIYO MENEJA WA MFUKO WA HIFADHI ZA JAMII AMESEMA HAYUKO TAYARI KUMFIKISHA MAHAKAMANI MUAJIRI YOYOTE ENDAPO TU ATATEKELEZA WAJIBUWAKE.

PIA AMEWAMBA WAJIRI WAACHE KABISA KUCHELEWESHA MICHANGO KWANI NIHAKIYAMSINGI KUPELEKA MICHANGO KWANI WATUMISHIWAO WANAWAFANYIKA WAWEZEKUPATA MAFAO YAO KWAWAKATI.
Baadhi ya wateja wakichangia hoja  katika semina hiyo.
 bi.Happines Manyenye,akitoa maswali kwawateja wake wa mfuko wa PPF jijini Mwanza.

 Bw.Mashack Bandawe,meneja wa PPF kanda ya ziwa akieleza faida za mfuko wa hifadhi za jamii PPF jijini Mwanza.
Maafisa wa mfuko wa ppf wakiwa kwenye semina jijini Mwanza. 
Meshack Bandawe akionyesha huduma mbalimbali PPF inazozitoa hapa nchini.  Taasisi mbalimbali wakiwa katika semina iliyoandaliwa na PPF.

Sunday, January 17, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye alifuta gazeti la Mawio kwa tuhuma za kuandika habari za kichochezi.https://youtu.be/3sBeUgEn4RI

Waumini wa dini kiislamu nchini watakiwa kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano ya dhidi ya rushwa na ufisadi.https://youtu.be/Yh0oQLChKBA

Jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia watu 85 wanaosadikiwa kuwa raia wa Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini bila vibali.https://youtu.be/XtwMPLCOjIg

Serikali yatangaza kusitisha uuzwaji wa nyumba zake ilizopangisha kupitia shirika la nyumba NHC amabazo hazipo kwenye miradi ya nyumba za mauzo ili kuhakikisha wananchi wa kipato cha chini wanaendelea kusaidiwa na serikali.https://youtu.be/6SKDPhV389M

Wakazi 45 wa mtaa wa Kchangani kata ya Majohe manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam wafanikiwa kupimiwa makazi yao na kupata hatimiliki ya makazi.https://youtu.be/enKlC6n2SDs

Kilio cha wachimbaji wadogo wa Madini katika halmashauri ya wilaya Chunya mkoani Mbeya kwa Rais Magufuli kuwasaidia eneo la uchimbaji chapata ufumbuzi baada ya serikali kuuamuru mmiliki wa mgodi wa Shanta kuondoka na kuwaachia wananchi. https://youtu.be/3SWT6C_fTcU  

BOT yaipa siku 20 benki ya Stanbic ya hapa nchini kujitetea kwanini isichukuliwe hatua kwa kufanya miamala yenye mashaka.https://youtu.be/-2W2KwJwp9U

Bunge la Jumuiya ya Afika Mashariki lauvalia njuga mgogoro wa Burundi huku kamati ya jumuiya ya EAC inayoshughulika na mgogoro ikitaka kukutana na serikali ya Burundi. https://youtu.be/PvQpDM5BNdE

Baraza la vijana la Chadema BAVICHA latishia kumshitaki msajili wa vyama nchini kama hatokichukulia hatua chama cha mapinduzi hatua za kinidhamu kufuatia wafuasi wa chama hicho kutoa ujumbe wa kibaguzi.https://youtu.be/Ko7eit5P9OA

Migogoro sekta ya ardhi yaendelea kuwa kaa la moto hapa nchini baada ya mtu mmoja kuuwawa na nyumba 44 kuchomwa moto kufuatia mgogoro wa ardhi wilayani Muleba mkoani Kagera. https://youtu.be/tDI9thnyA0A

Serikali yapiga marufuku kwa watendaji wa maliasili nchini kuharibu mali za wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi na badala yake kutoa elimu kuhusu sheria ya misitu kwa wananchi. https://youtu.be/NxgSNZ4kJNQ  

Benki kuu ya Tanzania yaiandikia barua benki ya Stanbic Tanzania kwa lengo la kuitoza faini baada ya kubaini miamara ya kutia shaka;https://youtu.be/QstLeQBXaJs  

Serikali wilayani Kasulu mkoani Kigoma imewataka walimu kurejesha fedha walizowachangisha wazazi wakati wa kuwaandikisha watoto shuleni;https://youtu.be/DhKMmOCYe4Q   

Mbunge wa jimbo la Segerea kwa tiketi ya CCM, Mhe. Bonna Kaluwa amezindua kampeni kwa lengo la kuboresha miundombinu ya shule na utoaji wa elimu bora  kwa wanafunzi; https://youtu.be/xrg4CCrvj0M  

Serikali imelifuta gazeti la Mawio katika daftari la usajili wa magazeti kutokana na kukiuka sheria ya vyombo vya habari; https://youtu.be/4LknCRI1iAk  

Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi aigiza serikali mkoani Morogoro kupitia upya orodha ya mashamba makubwa yaliyowekwa rehani ili kujiridhisha kama yanaendelezwa; https://youtu.be/KOgJdfSfJog  

Timu ya Yanga yamaliza mgogoro uliokuwepo baina yake na mchezaji wa kimataifa Haruna Niyonzima baada ya kukiri kosa na kuomba msamaha;https://youtu.be/T4nFy1vwohY  

Timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa goli 1 kwa 0 dhidi ya timu ya Ndanda ya mkoani mtwara katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara;https://youtu.be/0TeGBPCTmpQ  

Serikali yavitoza faini viwanda viwili vya mkoani Morogoro kwa kukiuka sheria ya mazingira; https://youtu.be/DnHE3lSjWxw
    
Waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba awachukulia hatua kali watendaji wa serikali na mawakala wa pembejeo mkoani Ruvuma kwa tuhuma ya udanganyifu; https://youtu.be/YYerUPkMWrc  

Serikali wilayani Hai mkoani Kilimanjaro yazifunga kambi za wakulima kufutia kulipuka kwa ugonjwa wa kipindupindu wilayani humo;https://youtu.be/oB5zo9qTF4I  

Baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya wasichana ya Rugambwa  mkoani Kagera wameiomba serikali na wadau kuwasaidia ujenzi wa miondombinu rafiki itakayozingatia mahitaji ya wanafunzi wenye ulemavu;https://youtu.be/WFfyq8CRP2w   

inaelezwa kuwa serikali imeanza kuangalia upya viwango vya kodi katika shirika la nyumba la taifa NHC; https://youtu.be/iuaYSiPRZgw  

Baadhi ya mashabiki wa timu ya Simba waelezea maoni yao kuhusu kiwango kinachooneshwa na timu yao; https://youtu.be/KZKmVJJZj88  

Kocha wa timu ya Everton, Roberto Martinez alalamikia goli lililofungwa na mchezaji wa Chelsea, John Terry kuwa lilikuwa la kuotea;https://youtu.be/WV8gOJrP-m8