Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukivuka mto kuelekea katika kijiji cha Ilyanchele wilayani Bukombe wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika wilaya hiyo kuelekea katika kijiji hicho hata hivyo msafara huo haukuweza kuvuka mto mkubwa wa Ilyanchele na magari kutokana na kutokuwepo kwa daraja linalounganisha kijiji hicho ambapo leo ndiyo limewekwa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo na Ndugu Abdulrahman Kinana.
Baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa daraja hilo Kinana pamoja na msafara wake walivuka mto huo kwenye daraja la miti lililotengenezwa kwa nguvu za wananchi. kisha alipanda pikipiki na kuelekea katika mkutano mdogo na wananchi wa kijiji cha Ilyamchele ambacho kimo katika msitu wa akiba kata ya Nyamonge wilayani Bukombe mkoani Geita.
Kinana yuko katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Kagera, Geita na Mwanza ambapo baada ya kumaliza ziara yake mkoani Kagera sasa anaendelea na ziara hiyo katika mkoa wa Geita kabla ya kumalizia ziara yake mkoani Mwanza akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akivuka na wananchi katika daraja hilo.
Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia mjini Bukombe,mkoani Geita
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwahutubi Wananchi katika mkutano wa hadhara mjini, Bukombe wakati wa ziara yake mkoani Geita.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akitema cheche katika mkutano wa hadhara mjini, Bukombe wakati wa ziara yake mkoani Geita.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiunguruma katika mkutano wa hadhara mjini Bukombe.
Wananchi wakimlaki Katibu Mkuu Kinana kwenye mkutano wa hadhara mjini Bukombe
Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa chumba cha darasa katika Shule ya Msingi ya Ilamchele, wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita.
Sehemu ya chumba cha darasa cha Shulre ya Msingi Ilyamchele, katika Kata ya Namonge, wilayani Bukombe. Ndugu Kinana baada ya kuona hali hiyo, aliitisha harambee ya ujenzi wa shule hiyo, isiyokuwa na walimu wataalamu
Ujenzi wa vyumba viwili vya darasa katika Shule ya Msingi ya Ilyamchele ukiendelea, wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitumia usafiri wa pikipiki alipokuwa anakwenda Kijiji cha Ilyamchele, Kata ya Namonge ambako aliendesha harambee ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Ilyamchele akiwa katika ziara wilayani Bukombe, Geita, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi cya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Wananchi wakivuka daraja la Ilyamchele wilayani Bukombe, Geita.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizindua ujenzi wa wa dara la Ulyamchele,wilayani Bukombe mkoani Geita.
Gari lililombeba Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye likivuka katika moja ya mito katika Kijiji cha Ilyamchele, wilayani Bukombe.
Msafara wa Komredi Kinana ukivuka katika moja ya mto iliyopo Barabara ya Ilyamchele.
PICHA NA MICHUZI JR -BUKOMBE
No comments:
Post a Comment