Sunday, June 14, 2015

DKT. MAGUFULI ATAPA WADHAMINI KATIKA MIKOA YA UNGUJA NA PEMBA, ZANZIBAR

Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mchakato wa uhakiki wa kadi za wanachama wa CCM Wilaya ya Mfenesini Kisiwani Zanzibar waliojitokeza kumdhamini. 
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho kutoka kwa Mussa Haji Katibu wa CCM Wilaya ya Mfenesini Kisiwani Zanzibar.
Dkt. John Magufuli akisomewa dua katika Wilaya ya Wete Pemba mara baada ya kumaliza zoezi la kupata wadhamini katika katika kisiwa cha Pemba. Dkt. Magufuli amepata Wadhamini katika mikoa mitano kisiwani Zanzibar, Mitatu Unguja na Miwili Pemba Picha namba 6. Zoezi la udhamini likiendelea katika eneo la Chakechake mkoa wa Kusini Pemba.
Dkt. Magufuli akifurahia mara baada ya kukabidhiwa fomu za Wadhamini kutoka kwa Katibu wa CCM wilaya ya Kaskazini B-Unguja. 
.Dkt. Magufuli akikabidhiwa fomu za wadhamini Wete Kisiwani Pemba.

No comments:

Post a Comment