Wednesday, September 30, 2015

MWIGULU NCHEMBA ASAKA KURA ZA CCM KATA KWA KATA,ATUA HAI,VUNJO,SAME,ARUMERU NA MWANGA

Wananchi wa Hai Mjini wakimpokea Mwigulu Nchemba kwa shangwe.Mwigulu Nchemba ameshawasili Hai Mjini kuzungumza na Wananchi na Kumuombea Kura Rais Mtarajiwa kutoka Chama cha Mapinduzi Ndg,J.Pombe Magufuli.Mwigulu Nchemba akitoa Darasa kwa Wananchi wa Hai Mjini kuhusu Umuhimu wa Kuchagua kiongozi kwa Malengo,sio kuchagua Uongozi kwa Kishabiki."Wanahai naomba Mmchague Magufuli kwasababu ndiye kiongozi anayeweza kushughulika na Matatizo ya Wananchi wetu hasa swala la Rushwa,Uzembe maofisini na wadhurumaji.Kwa hapa Hai mmeshaonja ubaya wa Upinzani,hawajishughulishi kwa maendeleo Zaidi ya kupiga kelele zisizokuwa na tija kwa Wanahai".Wananchi wa Hai wakisema Nguvu Moja.Mwigulu Nchemba akiwasili USA river hapo jana.Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya CCM Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa USA River mapema hapo jana.Mbunge mtarajiwa wa Moshi Mjini Ndg.Davis Mosha akisalimiana na Mwigulu Nchemba wakati wa Mkutano wa hadhara ndani ya kata ya Sokoni.Mwigulu Nchemba akimnadi Davis Mosha mbunge Mtarajiwa kwa Moshi mjini.Mwigulu Nchemba akiwasili Same Mashariki.Mwigulu Nchemba akimnadi Mbunge mtarajiwa wa Same Mashariki Bi.Anna Kilango Malecela mapema hii leo wakati alipokwenda kuinadi Ilani ya CCM.Comrade Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Same Mashariki kuhusu Umuhimu wa kufanya Uchaguzi kwa Amani,Pia kuichagua CCM kwasababu imefanya kazi kubwa kuiletea Maendeleo Nchi yetu,Kwa Same serikali ya Magufuli nakwenda kujenga Barabara kwa kiwango cha Rami kuelekea Nkomanzi na Same Mashariki.Wananchi wa Mwigulu Nchemba akimndai Mathayo David Mgombea Ubunge Jimbo la Same Magharibi.Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Vunjo kupitia CCM Ndg.Innocent Shirima hii leo.Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Vunjo kuwa Mabadiliko sio vyama,Mabadiliko ni shughuli za maendeleo na Utendaji kazi.Magufuli anakwenda kubadilisha Utendaji kazi na Usimamizi wake. Picha na Sanga R.

MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AENDELEA NA MIKUTANO YAKE YA KAMPENI KATIKA VIWANJA CHA GARAGARA MTONI ZANZIBAR,

Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein. akisalimiana na Viongozi wa CCM alipowasili katika viwanja vya garagara mtoni kwa ajili ya kuendelea na mikutano yake ya kampeni Zanzibar kuomba ridhaa za Wananchi kumchagua tena kuongoza Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohameid Shein, akisalimiana na Mama Fatma Karume alipowasili katika viwanja vya garagara mtoni kwa ajili ya mkutano wake wa kampeni.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Ndg Yussuf Mohammed akizungumza na Wananchi na WanaCCM katika viwanja vya garagara mtoni wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, na kuwatana Wananchi kumpigia kura Dk Shein, ili kuzidi kuleta maendeleo katika Visiwa vya Unguja na Pemba katika kipindi cha miaka mitano ijayo. 
Wanachama wa CCM wakiwa katika viwanja vya garagara wakihudhuria mkutano wa kampeni ya mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, 
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urai kupitia CCM katika viwanja vya garagara Mtoni Zanzibar. 
Mama Fatma Karume akiwahutubia Wananchi wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viiwanja vya Garagara mtoni Zanzibar na kuwataka siku ikifika kutia kura ya Ndio kwa Dk Ali Mohamed Shein, 
Wananchi wakimshangilia Mama Fatma Karume wakati akiwahutubia katika mkutano wa Kempeni ya Mgombea ya Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Wasaani wa Bendi ya Moto wakitowa burudani kuhamasisha  Wanachama wa CCM wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, zilizofanyika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Mambo ya Yomoto Bendi hayo katika viwanja vya mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk Ali Mohamed Shein, iliofanyika katika viwanja vya garagara wakimuombea Kura Dk Shein, wakati wa kampeni yake.  

Wanachama wa CCM wakifuatilia burudani hiyo wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea wa Urais wa Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi na Wanachama wa CCM katika viwanja vya garagara mtoni akiwa katika mikutano yake ya kampeni ya kugombea Urais wa Zanzibar. kwa kupata ridhaa za Wananchi kuongoza Zanzibar kwa Maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar katika sekta mbalimbali na kudumisha Amani na Utulivu katika Visiwa vya Unguja na Pemba. 

Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa Mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar na kutowa sera za CCM kwa kipindi cha miaka mitano ijayo ya kipindi chake baada ya kupata ridhaa za Wananchi kumpa kura ya Ndio.katika uchaguzi mkuu mwa huu.
Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi akifuatilia Sera za CCM wakati Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa mkutano wake wa kampeni katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar
Wanachama wa CCM wakifuatilia Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya garagara mtoni 

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Welezo Zanzibar kupitia CCM Saada Mkuya katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtoni Zanzibar wakati wa mkutano wa kampeni za Urais wa Zanzibar Dk Shein katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mfenesini Zanzibar Kanali Mstaaf Khamis , wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Uwakilishi wakati wa mkutano wa kampeni za Urais zilizofanyika katika viwanja vya garagara Zanzibar.
Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Mfenesini Zanzibar Mhe Machano Othman akizungumza kwa niaba ya wagombea wezake katika mkutano wa kampeni ya Urais wa Zanzibar uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea wa Udiwani wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.


Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohameid Shein, akiagana na Viongozi wa CCM baada ya kumalizika kwa mkutano wa Kampeni katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar 
Imetayarisha na OthmanMapara.Blogspot.

WAKAZI WA DUNGUMBI WAAIDIWA KUTAKULIWA TATIZO LA MAJI

 Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan akizungumza wakati akinadi sera za chama Cha Mapinduzi,CCM  mbele ya wanaCCM wa mtaa wa Kisiwani, Kata ya  Ndugumbi jana jijini Dar es Salaam na kuaidi kuwa endapo atachaguliwa kurudi katika kiti chake kuwa atatatua tatizo la maji linalowakabili wananchi wa kata hiyo.
  Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan akiwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kinondoni, Marry Kalisinje wakati  wakati mbunge wa Kinondoni akinadi sera zake katika  mtaa wa Kisiwani, mtaa wa Ndugumbi jana jijini Dar es Salaam. 

 Kushoto ni Mgomea wa Udiwani wa kata ya Ndugumbi, jimbo kinondoni a ya  kwa tiketi ya chama cha CCM,Thadey Massawe akionyesha Ilani ya chama hicho mara baada kupewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kinondoni, Marry Kalisinje.

Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan akiwa na wajumbe wa CCM.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan.

NAMELOK SOKOINE AZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE MONDULI AHIDI KUENDELEZA ALIPOISHIA LOWASSA

MGOMBEA jimbo la Monduli kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine, akihutubia mkutano wa hadhara wakati wa uzinduzi wa kampeni zake zilizofanyika katika viwanja vya Nanja Mnadani Monduli mkoani Arusha Septemba 28,2015 ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi kuendeleza yote aliyoasisi, kusimamia na kutekeleza aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Edward Lowassa.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro akihutubia mkutano wa  uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Namelok Sokoine akihutubia wananchi katika mkutano huo wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni zake.
 Namelok Moringe Sokoine akiwasili katika uwanja huo wa Nanja tayari kwa uzinduzi wa kampeni.
 
Wazee wa Kimila wa Jamii ya Kimaasai wa Monduli wakiongoza dua maalim ya kumuombea Binti yao Namelok.
 Mwalimu Lorinyu Nkoosi, mmoja wa waliochuana na Namelok Sokoine katika mchakato wa uteuzi ndani ya CCM akiongea. 
 Wananchi wa Monduli wakiwa katika mkutano huo.
Wajane wa Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine ambao ni mama za Namelok Sokine wakitambulishwa mkutanoni hapo na Mwenyekiti wa kamati ya kampeni za CCM jimbo la Monduli, Paul Kiteleki.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro (kulia) akimkabidhi ilani ya Chama cha Mapinduzi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine wakati wa uzinduzi wa jkampebni zake uliofanyika Monduli jana.
 Dk Asha-Rose Migiro akisalimiana na wamama wa kimaasai alipowasili mkutanoni hapo.