Friday, June 12, 2015

MAKAMBA AITIKISA RUVUMA, UDHAMINI WA WATU 3550 WAVUNJA REKODI

 Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Bumbuli, January Makamba amewataka makada wote waliomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya urais ndani ya Chama  kuwa wanakiacha chama hicho kuwa salama baada ya mchakato huo kukamilika.

January, aliyasema hayo baada ya kupokea orodha ya wanachama wa chama hicho, katiaka Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa Ruvuma jana, ambapo wanachama 3500 walijitokeza kumdhamini.

Alisema hivyo kwa vile kuna wapo waomba ridhaa ambao wanadai kuwa endapo hawatateuliwa katika nafasi hiyo kuna hatari chama kikasambaratika.

Alisema, chama hicho kinahitaji kupata mgombea ambaye atahakikisha kuwa nama hicho kinabaki salama na kwambapia atawaongoza watanzania wote bila kujali dini wala kabila zao, akibainisha kuwa yeye ndio sahihi katika kudumisha hayo.

 ”Mimi siamini siasa za kupakana matope kwani wote ni wanachama wa chama kimoja na mwisho wa siku tutapata mgombea mmoja na tutahitajika kumpigia kampeni”alisema Jamuary.

January, alisema kama wagombea watapakana matope katika mchakato huo wa kuomba ridhaa kwa wanachama, anaamini wakati ukifika wa kumfanyia mteule utakuwa mgumu kwani itakuwa siyo rahisi kumfanyia kampeni ambaye tayari umekwisha kumpaka matope.

“Niwaombe muwapime wagombea ambao wameonekana wakiomba nafasi hiyo kwa mbwembwe kwani hatawatakapopata nafasi hiyo wataongoza kwa mbwe jambo ambalo wananchi hawalihitaji”alisema Jamnuary.

January, alisema kuwa chama hicho kiko makini na hakitamteua mgombea kwa woga kama inavyodaiwa na baadhi ya wagombea  kwamba wasipochaguliwa chama hicho kitasambaratika jambo ambalo siyo sahihi.

Alisema kuwa anaamini kuwa chama hicho kitamteuwa mgombea ambaye ni muadilifu, atakuwa rahisi katika kumnadi kwa wananchi.

Akizungumzia, mkoa wa Ruvuma, January, alisema mkoa huo hivi sasa unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la umeme na upande wa hospitali ya Mkoa.

Alisema kwa vile matatizo hayo anayatambua, pindi atakapopewa ridhaa na chama na kuchaguliwa kuwa rais atahakikisha mkoa huo unaingizwa katika gridi ya Taifa kama ilivyo kwa mikoa mingine.

Katika hatua yingine, juzi mkoani Njombe, January alipata wadhamini 84.

January, alisema anaamini atakapokuwa rais atakuwa na uwezo wa kuamua mambo makubwa yanayolihusu taifa ukilinganisha na nafasi aliyosasa kwani inamopaka katika maamuzi ya kushughulikia mambo mbalimbali ya Taifa. 


Mh January Makamba akihutubia wanachi na wanachama wa CCM mkoani Ruvuma mara baada ya kabidhiwa fomu yenye sahihi za wanachama waliomdhamini.
Mh January Makamba akihutubia wanachi na wanachama wa CCM mkoani Ruvuma ndani ya ukumbi wa ofiswi kuu ya chama hicho mkoani Ruvuma. kuanzia kushoto ni mke January Makamba, Ramona Makamba, katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma, Verena Shumbusho na kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa, Odo Mwisho.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma, Odo Mwisho akimkabidhi fomu yenye majina na sahihi za wanachama waliomdhamini mh. January Makamba. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano katika ofisi kuu ya CCM mkoa wa Ruvuma


 Mh January Makamba na mkewe, Ramona Makamba wakipeana mikono na wanachama wa CCM mkoa wa ruma waliofika katika ukumbi wa  mikutano katika ofisi kuu ya CCM mkoa wa Ruvuma.
Katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma, Verena Shumbusho akiwakaribisha mkoani Ruvuma Mh January Makamba na mkewe.

No comments:

Post a Comment