Saturday, June 20, 2015

WAZIRI BERNARD MEMBE AWASILI BUKOBA KUSAKA WADHAMINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akishuka kwenye ndege katika uwanja wa Bukoba hii leo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe ametua Bukoba leo hii Jumamosi jioni Kutafuta wadhamini ambapo pamoja na mambo mengine amesema kuwa katika siku za hivi karibuni alipochukua fomu ya kugombea Urais, Kuna baadhi ya watu wakiwemo wenye fedha chafu na wafanyabiashara wanamfuata fuata na kumuomba eti wanataka kumsaidia katika mchakato wa urais."Nawaambia kuanzia leo wakome kunifuata fuata" amesema Waziri Membe. Amepata wadhamnini 534 kutoka Wilaya za Bukoba Mjini na Vijijini. Picha zote Faustine Ruta, Bukoba.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akisalimiana na Baadhi ya Viongozi waliofika Katika Uwanja wa Ndege kumpokea.
Utambulisho Ukiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiongozana na Umati wa Watu kutoka Uwanja wa Ndege mpaka Zilipo Ofisi kuu za CCM hapa Bukoba Mjini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akisindikizwa na Vijana Machachari wa Chama cha CCM kuelekea makao Makuu ya ofisi za CCM.
Furaha ya mapokezi
Bernard Membe akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za CCM Mkoa wa Kagera
Bernard Membe akiongea na wananchiUmati wa Watu wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe wakiwemo na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wa hapa Mkoani Kagera, waliofika katika Ofisi ya CCM ya Mkoaleo juni 20, 2015 kwa ajili ya kumdhamini iliaweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500.

No comments:

Post a Comment