Thursday, June 11, 2015

LOWASSA APATA WADHAMINI ZAIDI YA ELFU SABA MKOANI SHINYANGA

Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na mtoto mwenye ualbino, Kabula Zacharia, anayetunzwa kwenye kituo cha kulea watu wenye mahitaji maalum cha Buhangija mkoani Shinyanga, mara baada ya kupata wana CCM wa kumdhamini kufuatia kuchukua fomu za kuomba chama kimteue kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa ambaye yuko kanda ya ziwa kutafuta wadhamini, alivunja rekodi ya kupata wadhamini 7,114, idadi kubwa hadi sasa. (Picha na K-VIS MEDIA)
Mh. Lowassa, akipokea fomu zilizojazwa na wana CCM waliomdhamini mkoani Shinyanga, kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Shin yanga mjini Charles Sangula, Juni 11, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akipungia mkono wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, alipokuwa akiondoka ofisi za chama hicho wilaya ya Shinyanga mjini mara baada ya kupata wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu kuomba CCM imteue kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amabaye yuko kanda ya ziwa kutafuta wadhamini, alivunja rekodi ya kupatya wadhamini 7,114, idadi kubwa hadi sasa. 

Furaha ya kumuona Mh. Lowassa, ilitawala ukumbi mzima



Wana CCM walkiofika kumdhamini Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, wakishangilia wakati akiingia ukumbi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Juni 11, 2015. Lowassa amabaye yuko kanda ya ziwa kutafuta wadhamini, alivunja rekodi ya kupatya wadhamini 7,114, idadi kubwa hadi sasa
Wananchi wa mkoa wa Shinyanga, wakisukumana ili wapiti kumuona Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, alkipokuwa akiwasili kwenye ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini Juni 11, 2015, ili kuomba wanachama wenzake wa chama hicho wamdhamini kufuatia kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na chama hicho, kuwania urais wa Tanzania Oktoba 25, 2015
Wana CCM walkiofika kumdhamini Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, wakishangilia wakati akiingia ukumbi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Juni 11, 2015. Lowassa amabaye yuko kanda ya ziwa kutafuta wadhamini, alivunja rekodi ya kupatya wadhamini 7,114, idadi kubwa hadi sasa

No comments:

Post a Comment