Waziri asiye na wizara maalum Prof Mark Mwandosya akiwapungua mkono
baadhi ya wahudumu wa uwanja wa Ndege wa Nduli Iringa wakati
akiondoka mkoani Iringa kuelekea mkoani Tabora kutafuta wadhamini kwa
ndege hiyo ya kukod
Waziri Prof Mwandosya akitafakari jambo |
Dereva wa gari alilokodi Prof Mwandosya Iringa na rubani wa ndege aliyokodi waziri huyo wakiagana |
Wadhamini wa Prof Mwandosya wakiagana na waziri huyo
Waziri Prof Mwandosya na mkewe akishuka katika gari la kukodi leo ofisi za CCM wilaya ya Iringa vijijini |
Waziri Prof Mwandosya akizungumza na wanahabari mkoa wa Iringa |
Mke wa waziri Prof Mwandosya ,katibu msaidizi wa CCM Iringa vijijini Bw Jackson na waziri Prof Mark Mwandosya wakisikiliza maswali ya wadhamini |
Baadhi ya wadhamini wa waziri Prof Mwandosya |
Katibu msaidizi wa CCM wilaya ya Iringa vijijini Bw Hakim Jackson (kushoto) akimkabidhi Prof Mark Mwandosya fomu yenye majina ya wadhamini wake mkoani Iringa |
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Iringa vijijini Shakra Kiwanga akimpongeza Prof Mwandosya |
Prof Mwandosya akiwaaga wadhamini wake |
Prof Mwandosya na mkewe wakiingia katika ndege tayari kwa safari ya kwenda mkoa wa Tabora na Kigoma |
Prof Mwadosya akifurahia kupata fomu ya wadhamini wake
Na MatukiodaimaBlog
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya ambae ni mmoja kati ya wana
chama wa chama cha mapinduzi zaidi ya 35 walijitokeza kuchukua fomu
za kuomba kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM
amesema kuwa baada ya mwaka 2005 kushika nafasi ya tatu katika
kinyang'anyiro cha Urais ni matumaini yake mwaka huu atafanya vizuri
zaidi kwa kushika nafasi ya kwanza kati ya wote waliojitokeza sasa.
"Wewe
una mtoto anasoma darasa la tatu mfano na darasa kati ya watoto
90 yeye amekuwa wa tatu ukiwa kama mzazi lazima utampongeza na
kumweleza kuwa uongeza jitihada na mtihani ujao baada ya kuongeza
jitihada kuwa mwanangu nataka mtihani ujao uwe wa kwanza sawa
anakujibu sawa ......sasa mimi mwaka 2005 nilikuwa wa tatu sasa
unataka kuniambia nini tena"alihoji Prof Mwandosya huku wote wote
pamoja na wanahabari wakiangua kicheko .
Akizungumza
na wanahabari leo katika ofisi ya CCM wilaya ya Iringa vijijini
mara baada ya kudhaminiwa na wanachama 28 wa CCM ,Prof Mwandosya
alisema kuwa safari yake ni safari ya uhakika na hivyo iwapo chama
chake kitamteua kuwa mgombea watanzania wategemee kuwa na nchi yenye
uchumi bora .
Prof
Mwandosya ambae aliulizwa na wanahabari hao kuwa anajambo gani
jipya la kulifanya ambalo Rais anayemaliza muda wake Dr Jakaya
Kikwete hakufanya alisema kuwa si kweli kama serikali ya Dr Kikwete
haikufanya lolote japo alisema kiwa awamu ina changamoto zake na kila
awamu imefanya mambo makubwa
"Kusema
unalinganisha na serikali iliyopo ni kama vile unataka kusema
serikali zilizotangulia hazikufanya lolote ama hazikufikia malengo
yaliyotarajiwa ukweli ni vipindi katika uongozi wa nchi ambavyo
vinatofautiana mfano miaka iliyopita mimi nikiwa waziri wa
mawasiliano na uchukuzi simu hizi za mikononi ambazo matumizi yake
ni makubwa hazikuwepo ila sasa kuna simu ambayo ni kamera ,Voice
recoda na pia ni kopyuta hiyo hiyo sasa huwezi linganisha miaka
hiyo na sasa na huwezi sema serikali iliyopita haikufanya ukweli
kila serikali imefanya kulingana na wakati wake."
Alisema
kuwa atafanya zaidi ya serikali iliyopita ama chini ya serikali
iliyopita bado si jibu la kumsaidia mtanzania kwani alisema katika
ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005 -2010 ujenzi wa chuo kikuu cha
Dodoma haukuwepo na wala haikuwa ni ahadi ya Rais Dr Kikwete ila
kutokana na kuna kuna haja ya kuanzisha chuo hicho serikali iliweza
kuadhimia na kufanikiwa kuanzisha chuo hicho ambacho ndicho chuo
bora nchini na Afrika Mashariki .
Hata
hivyo alisema kuwa kwa kuwa kipaumbele chake kikubwa ni kujenga
uchumi bora pia ana amini kupitia uchumi bora hakuna jambo
litakaloshindikana kwani katika uchumi bora itakuwa ni vigumu
kuzungumzia uchumi bora kama miundo mbinu haitaboreshwa wala bila
kuwepo kwa kilimo na masoko ama kuwa na masoko bila viwanda au
kuzungumzia kukuza uchumi bila kuwa na elimu bora .
Prof
Mwandosya alisema kuwa mbali ya kuwa ni waziri ila bado anaishi na
jamii na pia anatambua mazuri mengi yaliyofanywa na Rais Dr Kikwete
na changamoto zake hivyo akiingia Ikulu lazima yale mazuri yote
yaliyofanywa na serikali iliyopita atayaendeleza zaidi ya hapo
yalipoachiwa na zile changamoto kuweza kuzitafutia majibu sahihi kwa
faida ya jamii ya kitanzania.
Pia
alisema mambo mengi anayatambua vema kwa kuwa yupo jikoni na
mengine anayatambua vizuri kutoka kwa jamii ambayo imemlalamikia hivyo
jukumu la kuyatekeleza lipo mikononi mwake na kuwataka wananchi hasa
wana CCM kuendelea kujenga imani zaidi kwake .
"
Lazima kuwa na vipaumbele ambavyo ni majibu ya mwananchi katika
kukuza uchumi kwani huwezi chukua elimu ukaacha miundo mbinu kwani
miundo mbinu ndio itakuza uchumi na huwezi zungumzia afya bila
kuboresha elimu ....ukifanya haya makubwa manne hapo ndipo unageukia
upande wa pili.....niseme tu kuwa uchumi unapokuwa lazima
unazungumzia takwimu na kuona kipato cha Taifa kinaongezeka"
Waziri
Prof Mwandosya alisema kuwa katika utawala wake kama Rais ni kuona
anakuza uchumi zaidi kupitia kilimo huku akiamini kuwa asilimia
zaidi ya 80 ya watanzania wanategemea zaidi kilimo katika kuendesha
maisha yao na kilimo pia kinaweza kukuza uchumi haraka zaidi .
Katika
hatua nyingine Prof Mwandosya amewataka wagombea wenzake kuheshimu
taratibu za CCM katika mchakato wa kutafuta wadhamini badala ya
kugeuza mbio hizo kama sehemu ya kuonyesha umarufu usio na tija na
kuwa utaratibu wa CCM ni kupata wadhamini 450 pekee pasipo
mbwembwe za aina yoyote pia vigezo vya mgombea wa urais wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania vipo wazi kuanzia kiwango chake cha elimu na
awe na miaka kuanzia 40 kuwataka wote watia nia kujitathimini badala
ya kuingiza mchezo katika suala hilo nyeti.
Prof
Mwandosya aliwataka wagombea wenzake ndani ya CCM wasilalamike kwa
kukumbushwa ukweli na madudu waliyoyafanya wakati wakiwa serikalini
kwani ni vigumu watanzania kusahau maovu ya mgombea yeyote na kuwa
anachojivunia yeye katika uongozi wake toka kipindi cha hayati baba wa
Taifa hadi sasa hajapata kuwa na sifa mbaya kama baadhi ya
wagombea wengine ambao wamechukua fomu ya kuomba kuaminiwa na CCM
mbali ya kuwa na sifa mbaya kwa Taifa .
Pia
alieleza kusikitishwa na matumizi makubwa ya pesa katika mchakato huu
na kuwa anashangazwa kuona wana CCM wakiendelea kuchezea pesa kwa
kuandaa mbwembwe nyingi mikoani kwa ajili ya mapokezi yao wakati kila
mgombea alipewa taratibu na chama juu ya nini afanye wakati wa
kuzunguka kutafuta wadhamini na kuwa pesa zinazotumia zingeweza
kusaidia miradi ya kijamii kuliko kuzimwaga kama njugu kwani ni hatari
kwa uhai wa chama .
No comments:
Post a Comment