Mgombea ubunge jimbo la Mafinga Bw Cosato Chumi kulia akisalimiana na mmoja kati ya wapiga kura wake |
Mgombea ubunge jimbo la Mufindi Kaskazin Bw Mahamudu Mgimwa akiwahutubia wananchi wakati wa mkutano wa Chumi
Mjumbe wa NEC Mufindi Marcelina Mkini akiomba kura za CCM
Mjumbe wa NEC Iringa Mahamudu Madenge akizungumza na wananchi wa jimbo la Mafinga
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mafinga Bw. Cosato
Chumi (CCM) amewataka wananchi wa jimbo hilo kuwa na iamani na kuwa wakimchagua atahakikisha anamulika kwa kutumia
tochi ubadhilifu katika sekta za elimu, afya, kilimo, barabara, maji na
kuhakikisha kuwa hakuna fedha ambazo zitatolewa na serikali kuleta maendeleo
kwa wananchi zitaliwa na watendaji ndani ya jimbo la Mafinga.
Hayo ameyasema jana wakati alipokuwa akijinadi kwa wananchi
wa jimbo la Mafinga katika Mtaa wa Bomani ambapo pia ulifanyika uzinduzi wa
kampeni za udiwani katika kata hiyo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu
pamoja na madiwani wote ambao wametangaza nia ya kuwania nafasi zao katika
jimbo hilo la Mafinga Mjini.
Bw. Cosato Chumi alisema kuwa wananchi wa jimbo la Mafinga ni
mashahidi wa shida zinazowapata na kuwakera wananchi ndani ya jimbo la Mafinga
Mjini ambapo alisema kuwa Hospitali ya wilaya kutokana na kuzidiwa na wagonjwa atahakikisha kuwa anapigania ili
kila kata kuwe na zahanati na katika tarafa za ndani ya Mafinga kujengwe kituo
cha Afya ili kupunguza msongamano wa wagonjwa.
Bw. Chumi aliongeza kuwa atapigania ili madawa na mahitaji
yote ya msingi kwa wananchi hususani wagonjwa kuwa yapatikane na kuhudumia
wananchi ambao kwa sasa kutokana na mlundikano mkubwa wa wagonjwa katika
Hospitali ya wilaya wagonjwa wanapoteza muda mwingi katika kutafuta matibabu ya
afya zao na familia zao.
“Nitahakikisha kuwa pesa zote za Umma za maendeleo
zinasimamiwa kikamilifu na hakuna ufujaji wa aina yoyote ile ambao utatokea na
kuongeza kuwa fedha zote zitakazotolewa ndani ya mfuko wa jimbo, pesa za
serikali za maendeleo pamoja na miradi mbalimbali zitamulikwa kwa umakini ili
zitekeleze shughuli ambayo imelengwa”, alisisitiza Bw. Chumi.
Alisema kuwa endapo viongozi wanategemea sana utendaji wa
kazi na shughuli za viongozi kutokana na kuwepo kwa umoja na mshikamano ambapo
alisema kuwa shule za sekondari zitahakikisha kuwa zinaendelezwa kila kata na
kuwahakikishia wananchi hususani watoto wao wanapata elimu sahihi.
Aidha, alisema kuwa mabweni katika shule za sekondari
yatahakikisha kuwa yanajengwa kwa malengo ya kuhakikisha kuwa wanafunzi
wanatulia shuleni na kusoma kwa utulivu ambapo alisema kuwa sekta ya elimu
inatakiwa ipewe kipaumbele ili watanzania wote waelimike na kuwezeshwa
kujitegemea na kujiajiri na kuajiriwa na sekta za binafsi na serikali kwa
manufaa ya kukuza uchumi ndani ya nchi.
Akizungumzia suala la kushughulikia usalama, Bw. Chumi
alisema kuwa atahakikisha kuwa anapigania kila kata ndani ya jimbo la Mafinga
linajengewa kituo cha Polisi ili kuwasaidia wananchi kulinda usalama na mali
zao, kuwasaidia wananchi endapo watahitaji misaada ya haraka kutoka kwa sekta
ya ulinzi wa jeshi la polisi ikiwemo mwananchi akipata ajali, akiibiwa,
akivamiwa na kupata misukosuko ya aina yoyote ile ambayo itahitaji jeshi la
polisi kuingilia kati kushughulikiwa kwa haraka.
JENGENI IMANI NA CCM KWA MAENDELEO ZAIDI - JIMSONI MHAGAMA
KATIBU wa CCM wa wilaya ya Mufindi Bw. Jimson Mhagama amesema
kuwa chama cha mapinduzi (CCM ) kitaendelea kuongoza kwa kuzingatia uadilifu, , amani,
upendo, utulivu na kuleta maendeleo kwa wananchi wake hivyo kuwataka wananchi
kuchagua cheni nyenye msimamo wa kuwa na diwani, mbunge na rais wa CCM ili
kuendelea kuwaletea maendeleo .
Bw. Mhagama aliitoa
kauli hiyo jana
alipokuwa akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni za
udiwani wa kata ya Bomani kwa kumnadi mgombea wa kata hiyo Bw. John
Chota ,kuwa wananchi waanze kumuunga mkono diwani, na mbunge
anayegombea wa CCM Bw. Cosato Chumi kumchagua kuwa mbunge wa jimbo la
Mafinga
Mjini pamoja na kuelekeza kura zote kwa
Mgombea wa Urais dkt. John Magufuli.
“Uongozi wowote wenye cheni moja ya kutoka chama kimoja ndiyo
unaoweza kuleta maendeleo na hivyo ninawaomba kura zenu mzielekeze kwa diwani
wetu John Chota, Mbunge wetu Bw. Cosato
Chumi pamoja na Rais wetu dkt. John Pombe Magufuli ili kuunda cheni moja ya
mshikamano na kutokana na uwepo wa cheni hiyo kutakuwa na mfumuko sahihi wa
maendeleo kwa wananchi katika sekta zote zikiwemo za elimu, kilimo, afya,
barabara, ujasiliamali, kutunza mazingira, ajira kwa vijana na uwezeshaji wa
akina mama”, alisema Bw. Jimson Mhagama.
Alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa cheni moja ya kimaendeleo
uongozi wa awamu ya Tano utakapoingia madarakani utahakikisha kuwa shule zote
za sekondari zinapatiwa umeme, kuendeleza ujenzi wa maabara, kuhakikisha
zinapatiwa walimu wa kutosha na kuongeza
kuwa elimu itatolewa bure kuanzia shule za msingi hadi sekondari kwa ajili ya
kuhakikisha kuwa watanzania walio wengi
ambao ni vijana wanaelimika na kunufaika na matunda ya nchi yao.
Aidha, alisema kuwa mara baada ya uchaguzi Jimbo la Mafinga
litahakikisha kuwa linajenga stendi kubwa ya kisasa ya mabasi yaendayo mikoani
ambayo yanapita katika Mji wa Mafinga
ambapo alisema kuwa ujenzi wa stendi hyo utagharimiwa na Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii wa LAPF ambapo stendi hiyo inatarajia kugharimu zaidi ya
shilingi Bilioni 3.5 na kuongeza kuwa utendaji huo utakwenda sambamba na
wananchi kuchagua cheni moja ya CCM na siyo kuleta mchanganyo wa wagombea.
No comments:
Post a Comment