Tuesday, September 15, 2015

CHAMA CHA ACT WAZALENDO WAFUNGUA KAMPENI ZA CHAMA HICHO IRINGA

 Mgombea  ubunge   jimbo la Iringa mjini  Bi  Chiku  Abwao.
Chiku  Abwao  akiwahutubia  wananchi 

Na MatukiodaimaBLog
CHAMA  cha ACT  wazalendo  kimezindua kampeni  zake  za  ubunge katika  jimbo la Iringa  huku  mgombea  wake ubunge  katika  jimbo  hilo Bi  Chiku  Abwao akivilalamikia baadhi ya   vyombo vya habari  nchini kwa  kukalia  habari  zake  zinazohusiana na uchafu  wa mgombea  Urais  wa  chama  cha  Demokrasia na maendeleo (chadema) anayewakilisha vyama vinavyounda  umoja  wa katiba ya  wananchi (UKAWA) Edward  LOwassa  kuwa hana sifa ya kuwa Rais wa nchini hii.

Akizungumza  wakati  wa uzinduzi  wa kampeni  zake  juzi katika  uwanja  wa Mwembetogwa  mjini Iringa , Abwao  alisema  kuwa anasikitishwa na hatua ya  baadhi ya  wanahabari na  vyombo  vya habari nchini kukalia pasipo  kuzitoa habari  za  kupinga  hatua ya Chadema na ukawa kumsimamisha Lowasa  kuwa mgombea  urais  wakati wao  kama   wapinzani sera  na ajenda yao  kubwa  ilikuwa ni  kupinga ufisadi na hata  kumtaja hadharani  waziri  mkuu  huyo  mstaafu kwenye  orodha ya mafisadi .

"Kila  wakati  nimekuwa  nikikemea hatua ya  Chadema na  Ukawa  kukumbatia mafisadi wakubwa na hata  kuwana nafasi  za  kuwania Urais  ila leo naomba kupeleka kilio  changu kwa baadhi ya  vyombo  vya habari na  wanahabari hapa  nchini ambao wamekuwa  wakikalia habari zangu za  kupinga  ufisadi  na kutoafiki mgombea  Urais wa UKAWA Bw Lowassa......nikikemea  sana  masuala ya  Lowassa  kuhusishwa na ufisadi papa na  Chadema na leo kukaribishwa  kugombea  Urais wanahabari na  vyombo  vya habari havitoi katika magazeti  ninawasiwasi na wao  wanamshiko  wa ufisadi nitasema  ukweli kwa  wale ambao wamemezwa  na ufisadi lakini  si kwa  wanahabari  na vyombo vyote  " alisema  Chiku

Kuwa  baadhi ya  vyombo vya habari na  mitandao ya  kijamii imekuwa ikitoa  habari  zake pasipo  kuficha  ukweli  ila wapo  baadhi  ambao  wamekuwa  wakificha  ukweli na yupo  tayari  kuendelea  kupinga hatua ya UKAWA  kumsimamisha  Lowassa  kuwa mgombea huku  akivitaka  vyombo  vya habari kulisaidia Taifa  kupata  kiongozi bora na  sio  bora   kiongozi.

" Wapo  baadhi ya  waandishi  wamekuwa  wakiweka mambo  wazi ila  wapo  ambao wamemezwa na ufisadi ambao kazi  yao ni  kutetea  ufisadi na kuwa  yupo  tayari  kusema  kweli kwa faida ya  watanzania "

Hata   hivyo  alisema  sababu ya  yeye  kuondoka  ndani ya CHADEMA ni  kutokana na hatua ya  chama   hicho  kumkaribisha  waliyemuita  fisadi  kuwa mgombea  Urais na  kuwaacha  wanachama  wenye  sifa  ya  kuliongoza Taifa .

Pasipo kutaja majina ya  wana chadema  ambao  walikuwa na sifa ya  kuwania nafasi ya Urais  alisema  kuwa kwa upande  wake  alikuwa ni mbunge  wa viti maalum na  mjumbe wa kamati kuu ya Chadema  ila kutokana na kukaribisha  watu  wachafu kugombea nafasi hiyo ya Urais hakupenda kubaki ndani ya  chama  hicho na  hivyo kulazimika  kujiunga na ACT  wazalendo  chama  chenye  misingi  bora ya  uongozi.

Bi  Abwao  alisema  kuwa kuna haja  ya  wananchi  kutomchagua Lowasa na pia kwa  wana Iringa mjini  kutoendelea  kuburuzwa na aliyekuwa mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa ambae  aliusadikisha  umma  kuwa Lowassa  ni fisadi na kuwa angewashangaa  watanzania ambao  watasimama  kumshangilia  Lowassa na hata kudai  kuwa  watu hao  wangepaswa  kupimwa akili ila  leo  yeye na viongozi wenzake wa UKAWA wamekuwa wa kwanza  kumpigia kampeni na  kunadiwa na huyo  waliyemuita ni fisadi hata  bila ya  kwenda  kupima akili  zao.

Alisema  kuwa lazima  wananchi  kukwepa  kuwachagua viongozi  wanaotafuta  ungozi kwa pesa na badala  yake kuchagua  viongozi makini  kutoka  chama  chake  cha ACT  Wazalendo ambacho hakina  ubia na mafisadi .

Kuhusiana na nini chama  chake  kitafanya  iwapo  wananchi  wa jimbo la Iringa mjini  watamchagua  kuwa mbunge wa  jimbo  hilo alisema ni pamoja na  kuweka mfumo mzuri wa  kuwasaidia  wazee kwa  kuwakatia  bima  za afya , kuanzisha miradi ya  vijana na  kusaidia  yatima  na  walemavu  kiuchumi.

Kwani alisema  mbunge  aliyekuwepo  jimbo  hilo Mchungaji Msigwa amechangia  kuua nguvu ya  upinzani katika   jimbo  hilo kutokana na kushindwa  kutimiza ahadi ambazo alipata  kutoa kwa  wananchi  mwaka 2010  japo ameomba  wananchi  kumwamini  yeye  kwa kumchagua  kuwa mbunge wa  jimbo  hilo japo kwa  kipindi  kimoja  cha miaka mitano na  iwapo atashindwa kutimiza ahadi  zake kama alivyofanya mchungaji Msigwa basi wasimchague  tena mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment