Thursday, September 3, 2015

LOWASSA ATUA MPANDA KWA CHOPA, APATA MAPOKEZI MAKUBWA

Chopa iliyowabeba Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mwenyekiti wake, Mh. Freeman Mbowe, ikitua kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili, Mpanda Mkoani Katavi leo Septemba 3, 2015.PICHA NA OTHMAN MICHUZI, KATAVI
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mwenyekiti wake, Mh. Freeman Mbowe, wakiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili, Mpanda Mkoani Katavi leo Septemba 3, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapingia wananchi wa Mpanda, Mkoani Katavi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akihutubia kwenye Mkutano huo wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili, Mpanda Mkoani Katavi leo Septemba 3, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akizungumza na Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku.
Furaha ya Vijana wa Mpanga.
Wanampanga wakiwa wameweka mikono juu kwa ishara ya kutaka Mabadiliko.
Baada ya kupigwa na jua kali, inabidi ajimwabie maji kupunguza ukali wa joto.

Mbunge aliemaliza muda wake wa Jimbo la Ole Zanzibar, Mh. Rajab Mbarouk akihutubia kwenye Mkutano huo.

Sehemu ya wanachana na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), waliofika kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia CHADEMA, Mh. Edward Lowassa.
Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrance Masha akizungumza na wananchi wa Mpanda.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mpanda Mjini, Jonas Kalinde akizungumza na wanampanda wenzake wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia CHADEMA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili, Mpanda Mkoani Katavi leo Septemba 3, 2015.
Wakisikiliza kwa Umakini.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akimkabidhi mfano wa funguo, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia kwenye Mkutano huo wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili, Mpanda Mkoani Katavi leo Septemba 3, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mpanda Mjini, Jonas Kalinde, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Urais, uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili, Mpanda Mkoani Katavi leo Septemba 3, 2015.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akizungumza jambo na Mgombea wa nafasi ya Udiwani katika Kata ya Mtapenda, Bi. Pauline Pesnacy, mara baada ya kumnadi kwa wananchi wa Mpanda, waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili, Mpanda Mkoani Katavi leo Septemba 3, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni na kunadi sera zake.

2 comments:

  1. OOOOOOOOHHHH WANA MPANDA HONGERENI KWA MAELFU NA MAELFU MLIOHUDHURIA MKUTANO WA MGOMBEA URAIS CHADEMA UKAWA LEO.AMA KWELI MMETIA FORA NI KALI YA AINA YAKE.USEMI KATIKA BANNGO LENU MOJAWAPO KATIKA MAMIA YA MABANGO ;MWANGA WA RADI HAUZUILIWI NA GIZA;LOWASSA IKULU MMEFUNGA KAZI BRAVO BRAVO BRAVO BRAVOOOOOO

    ReplyDelete
  2. 1. Umati unahitajika ku be translated into votes. hivyo hamasisheni kwa nguvu wananchi waende kupiga kura. Umati uwe wa UKAWA au wa Vyama vingine ni muhimu wahamasishwe waende kupiga kura. Ndio demokrasia yenyewe.

    2. Je UKAWA inaliangaliaje suala la majina ya waliojiandikisha kuwa kweli yapo kwenye daftari la wapiga kura. Isije ikatokea mwananchi amejiandikisha na ana cheti cha kupigia kura, lakini siku ya kupiga kura jina lake halipo na anaambiwa hawezi kupiga kura simply because jina lake halipo kwenye daftari. Hapo ndipo vurugu zinaweza kutokea. Isije ikatokea waliopo kwenye daftari ni watu wa upande mmoja na kuzuia watu wa upande mwingine kutopiga kura.

    3. Mpaka sasa kampeni ni za kistaarabu kwa pande zote zilizopo kwenye kingayanyiro cha uongozi. Ustaarabu huu wa hoja uendelee. Lakini palipo na takwimu sahihi zitolewe kuunga mkono hoja. Kama upande wako unahusika na hoja ya Richmond toa maelezo wacha kuficha maelezo, kama zipo hoja za EPA, BOT, ESCROW, Mermeta, Fedha za Mboga tu nk, eleza hoja na wahusika wananchi wapate habari, mnaficha nini, na lini mtazielezea kwa wananchi waweze kuchambua mambo.

    4. Hoja ya mifano ya Misri na Libya, UKAWA isemeeni msikae kimya, si mifano sahihi, inapotosha na kutia woga wananchi. Kwa nini msitumie mfano wa vyama kuungana Kenya na kusaidia kuleta mabadiliko. Sasa hivi Kenya ni rahisi kwa chama chochote kushika dola. Kwa sababu vyote sasa viko level moja. Hakuna chama kikubwa kushinda wengine. haya ndio mabadiliko wapiga kura wanataka. Kuwa na uwezo wa kuchagua chama kinacho deliver, na kama haki deliver kinapigwa chini. Na hii inawezekana tu kwa kupunguza nguvu ya hati miliki ya dola kwa chama kimoja. Mifano ya vurugu za Rwanda na Burundi wakati wa uchaguzi uliopita uliathiri maamuzi ya wananchi kwa woga wa kitu ambacho hakikuwa sahihi na hakiwezi kutokea kwetu. Hivyo hivyo mfano wa Misri na Libya unahitajika kufafanuliwa na UKAWA wapiga kura wasiingiziwe hoja ya hofu. jambo likiingizwa mara nyingi kwenye akili, akili inalichukulia kama kweli kumbe si sahihi.

    4. Baba wa Taifa ni Baba wa wananchi wote, hivyo hotuba zake zinaweza kutumiwa na wananchi wake. Tumieni speech zake katika matangazo ya Jingo kwenye TV, hususan mabadiliko yasipopatikana ndani ya chama tawala , yatapatikana kwa chama kingine. hakuna mwenye hati miliki wa baba wa Taifa, speeches zake ni mali ya wote, UKAWA zitumieni zinaleta uzito kwa wapiga kura. Mbona hatuwaoni UKAWA kwenye matangazo ya TV ( ITV, Star TV, Channel 10 , AZAM) hususan kwenye Prime Time kabla na baada ya Taarifa ya habari, au mmeshidwa kulipia kama tunavyoelezwa na kusikia kutoka kwa vyama vingine, au mmekosa nafasi.

    6. Endeleeni na kampeni za kistaarabu. Fujo kwenu iwe mwiko.

    7. Msisahau kuwapongeza Chama Tawala wanapofanya kampeni za kistaarabu, kama vile kutohodhi muda wote wa vipindi vya TV nk. Ndio ukomavu wa siasa huo. Siasa sio ugomvi, ni HOJA

    ReplyDelete