Tuesday, September 15, 2015

MH. IDDI AZZAN AZINDUA KAMPENI JIMBO LA KINONDONI JIJINI DAR

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge (kushoto) akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Mh. Iddi Azzan(kulia) mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya  CCM Mwinjuma Mwananyamala jana jioni.a , wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam.(Picha na Geofrey Adroph waPamoja blog)
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Mh. Iddi Azzan akizungumza na wananchama na wananchi wa maeneo mbalimbali ya jimbo la Kinondoni waliofurika katika viwanja vya  CCM Mwinjuma Mwananyamala jana jioni wakati wa uzinduzi wa kampeni
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akihutubia umma uliohudhuria uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CCM.
 Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa akimwaga sera za CCM mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika wakati wa ufunguzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Kinondoni zilizofanyika waliofurika katika viwanja vya  CCM Mwinjuma Mwananyamala jana jioni.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akiwasalimia pamoja na kutoa neno kwa wananchama na wananchi waliofika kwenye mkutano huo wa ufunguzi rasmi wa kampeni za mgembea Ubunge jimbo la  Kinondoni .
Mgombea udiwani kata ya Mwananyamala Bw. Songoro Mnyonge(kushoto) akitambulishwa kwa wananchi na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge(kulia)
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge  akimtambulisha Mgombea udiwani wa kata ya Kijitonyama,  Ndg. Kamugisha wakati wa ufunguzi wa kampeni za Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni
Mgombea udiwani kata ya Tandale Bw Tamimu akitema vidonge kwa wapinzani.
Bw. Massawe ambaye ni mgombea udiwani kata ya Ndugumbi akizungumza jambo wakati wa mkutano huo
 Mgombea Udiwani kata ya Magomeni Ndugu Bujugo akiwaomba kura wananchi waliofika kwenye mkutano huo na pia kuwapigia wabunge pamoja na raisi kupitia chama cha CCM
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge (kushoto) akipokea kadi ya CUF toka kwa bibi  ambaye alikuwa ni kada wa chama hicho alidai hajaona manufaa yeyote kuwepo katika chama hicho ambapo alijitoa rasmi na kurudi CCM.
Bibi akiwasalimia wananchama na wananchi waliofika kwenye mkutano huo
Mzee Dalali akihutubia mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo ambao mwenyewe alidai umati ulifikia watu laki 250.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Mh. Iddi Azzan akiendelea kumwaga sera
Umati mkubwa ukishangilia wakati wa mkutano

Baadhi ya wananchi waliofika kwenye mkutano huo


Wasanii wa kizazi kipya Tundaman na Bonge la Nyau wakitumbuiza mara baada ya Mkutani kwisha
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Mh. Iddi Azzan akiaga mashabiki wake baada ya kumaliza kuhutubia katika viwanja vya  CCM Mwinjuma Mwananyamala jana jioni.

No comments:

Post a Comment