MGOMBEA Ubunge wa jimbo la
Iringa Mjini kupitia ACT Wazalendo Bi Chiku Abwao(pichani) amesema heri ya miaka
mitano ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mobica Mbega ( CCM) kuliko
miaka mitano ya Mchungaji Peter Msigwa ( Chadema)hivyo ametawa mwaka huu
wananchi kumchagua yeye
Akizungumza
katika mkutano wake wa kampeni za Ubunge jana kata ya Kihesa alisema
iwapo atakuwa mbunge wao atahakikisha anakuwa mbunge wa mfano wa
kuwaletea maendeleo sahihi.
Kwani
alisema kuwa historia ya jimbo hilo mwaka 1995 walichagua NCCR mageuzi
ambapo Bw Mfalamagoha Kibasa kuwa mbunge ila baada ya kushindwa
kutekeleza ahadi zake mwaka 2000 walimchagua Monica Mbega ( CCM) ambae
kipindi cha kwanza alifanya Kazi vizuri na mwaka 2005 wananchi
walimchagua tena ila hakuweza kufanya Kazi ndipo walipomchagua Mchungaji
Peter Msigwa( Chadema) ambae hajafanya Kazi yoyote.
Hivyo
alisema kwa sasa imani yake juu ya wanaume kuwa wabunge katika
jimbo hilo haipo tena kwani hawana nia ya kweli ya kuwatumikia
wananchi na kudai kuwa iwapo mbunge aliyemaliza muda wake
mchungaji Msigwa angetekeleza ahadi zake vema leo asingesimama
kugombea ubunge bali angemuunga mkono mbunge huyo ili aendelee
kwa kipindi cha pili ila kwa kuwa hakuna jipya alilolifanya hana
imani nae na hivyo ni wakati wa wananchi wa jimbo hilo kuwapima
wagombea wengine waliojitokeza nje ya mbunge huyo .
Alisema
ahadi za mbunge aliyemaliza muda wake zilikuwa zaidi ya 14
ikiwemo ya kuwawezesha wananchi waliojiunga katika vikundi kupatiwa
mitaji ya kuanzisha biashara kwa wakati huo alisema yeye si
mbunge wa kutoa pesa bali atawawezesha kiuchumi kwa kuwapa nyavu
(mitaji) ila baada ya kuwa mbunge alianza kuwasema vibaya wananchi
kwa kudai yeye si mbunge wa kutoa pesa (ATM)pia aliahidi ujenzi
wa soko la kisasa Kihesa na kumweka mwanasheria katika ofisi
yake ila hadi sasa hakuna alichofanya na akikumbushwa hukimbilia
kujenga chuki na kila mtu .
Bi
Abwao ambae amepata kuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa
na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia Chadema alisema
kuwa hali ya chadema na UKAWA kwa sasa imepoteza mwelekeo na chadema
kugeuka ni chama cha kutetea mafisadi tofauti na iliyokuwa awali
kuwa chama cha kupinga ufisadi .
Hivyo
alisema sababu ya kukihama chama hicho na kujiunga na ACT
wazalendo ni kutafuta chama cha upinzani makini ambacho atawatumikia
wananchi bila ya kuwajengea maswali kama ilivyo hivi sasa kwa
mgombea wa Chadema Iringa mjini mhungaji Msigwa ambae alikuwa mbele
kupinga ufisadi na hata kusema wanaomuunga mkono aliyekuwa waziri
mkuu Edward Lowassa ambae ni mgombea wa Chadema kwa sasa wakapimwe
akili zao .
Alisema
Chadema kwa sasa imekuwa ni chama cha kupiga dili akiwemo
aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Msigwa ambae leo kati ya
maswali magumu ambayo anahojiwa na wapiga kura wake ni juu ya
kauli yake dhidi ya wale wanaomuunga mkono LOwasa kutakiwa kupimwa
akili zao.
Akielezea
kuhusu sera zake kwa wananchi wa jimbo la Iringa mjini iwapo
watamchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha anautumia vema
mfuko wa jimbo kwa kuwasaidia wazee ,vijana na wanawake kuwa na
vikundi vya kiuchumi tofauti na ilivyokuwa awali miaka mitano
iliyopita kwa mfuko huo kushindwa kufanya kazi yoyote.
Pia
kuhakikisha anaibana serikali ili vijana kupewa mikopo nafuu na
kuzuia posho kwa watumishi wa umma ambazo zimekuwa zikikwamisha
maendeleo katika jimbo hilo .
No comments:
Post a Comment