Na matukiodaima Blog MGOMBEA Ubunge wa jimbo la Iringa kupitia chama cha mapinduzi ( CCM) Frederick Mwakalebela amesema jimbo la Iringa Mjini limekosa kunufaika na fursa za maendeleo kwa kuwa halikuwa na mbunge makini wa kuleta maendeleo .
Hivyo amewataka wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kuecha kujutia kukosa maendeleo na badala yake kumchagua kuwa mbunge wao ifikapo Octoba 25 mwaka huu.
Mwakalebela ametoa kauli hiyo leo wakati wa mkutano wake wa kampeni za Ubunge kwenye kata ya Mshindo alisema iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha anasogeza maendeleo ya haraka kwa wananchi wa Jimbo la Iringa ambao kwa miaka mitano wamekosa kupata maendeleo hayo .
Kwani alisema hakuna sababu ya kujutia na badala yake kutumia nafasi hiyo kujutia miaka mitano ambayo wamepumzika pasipo kushuhudia maendeleo yoyote katika jimbo hilo la Iringa mjini.
Kuhusu nini atafanya baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge alisema ni pamoja na kuboresha miundo mbinu ,kuanzisha saccos ya vijana ,kuanzisha mfuko wa elimu wa jimbo kwa kutumia sehemu ya mshahara wake ,kuwawezesha wazee kupata matibabu ya bure na kuboresha sekta ya michezo.
Wakati aliyekuwa Mgombea Ubunge katika mchakato wa kura za maoni Balozi Augustino Mahiga alisema matumaini mapya ya jimbo la Iringa yatapatikana kwa kuchagua diwani ,mbunge na Rais toka CCM .
Kwani alisema kuwa majuto ya wanajimbo la Iringa ambayo wanayo kwa sasa ni kutokana na kukosa mbunge Makini wa kuwatumikia wananchi na badala yake kuwa na mbunge wa maandamano na fujo bungeni.
|
No comments:
Post a Comment