Na Mwandishi Wetu, Muheza
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya
Chama Cha Mapiduzi (CCM), katika jimbo la Muheza mkoani Tanga, Balozi Adadi
Rajabu (Kulia akipokea fomu), amesema atapigana kufa na kupona kuingiza wawekezaji wilayani humo
katika nyanja ya kilimo na utalii.
Akizungumza baada ya kunadiwa na
mgombea urais wa CCM, John Pombe Magufuli, Adadi amesema mjini hapa jana kwamba
ataelekeza nguvu kubwa katika kuvutia wawekezaji ili kuiinua Muheza kiuchumi.
Magufuli, aliyemnadi Adadi kwa
kumuita “tunu ya Wanamuheza”, alisema akichaguliwa na kuungwa mkono Adadi ni mtu mwenye hazina ya uzoefu adimu na mwenye kuaminiwa na watu na
taasisi nyingi ndani na nje ya Tanzania.
Kwa safi hizo ahadi zake ni rahisi kutekelezeka na kuinua maisha ya wananchi wa Muheza..
Adadi akieleza vipaumbele vyake
na mkakati wake wa kuboresha maisha ya watu kiuchumi na kijamii, aliahidi kupigania kukuza fursa za utalii na
kuwepo kwa viwanda vya kusindika muhogo
na matunda, mazao yanayopatikana kwa wingi Muheza.
Adadi, ambaye ni mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya
jinai mstaafu na balozi mstaafu, alitaja vivutio vya utalii kuwa misitu na viumbehai
katika milima ya Amani, na kuongeza kwamba atapigania
uimarishaji wa barabara kutoka Pangani hadi Muheza.
Amesema machungwa yanazalishwa
kwa wingi Muheza na mengi uharibika kwa kukosa soko la ndani na nje. “Hili
lazima tulifanyie kazi,” aliahidi, na kuwataka wananchi wachape kazi kwani
viwanda na masoko hudumu kwa kupokea mahitaji yasiyokatizwa kwa msimu mzima.
Muhogo na mtama ni mazao ya
chakula ambayo Umoja wa Mataifa unahimiza yalimwe kwa wingi na kusindikwa ili
kupambana na tatizo la njaa barani Afrika.
Adadi amewasihi wananchi wa Muheza kuilinda
amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, kwani pasipo amani hata
uchaguzi wenyewe unaweza kuingia dosari.
Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na
Madiwani utafanyika tarehe 25 Octoba mwaka 2015
No comments:
Post a Comment