Monday, September 7, 2015

MARY NAGU UZINDUA KAMPENI ZA CCM ARUSHA






SAM_5821Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera Mahusiano na Uratibu Dkt.Mary Nagu akimnadi mgombea Ubunge pamoja na madiwa katika uzinduzi wa kampeni jimbo la Arusha mjini tarehe 5/9/2015 katika uwanja wa soko kuu jijini Arusha(Picha zote na Pamela Mollel wa jamiiblog Arusha)
SAM_5835Umati wa watu uliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za ccm jimbo la Arusha mjini katika ene la soko kuu jijini Arusha,ambapo rasmi walizindua kampeni za ubunge na udiwani
SAM_5823Mgombea ubunge jimbo la Arusha mjini kupitia chama cha mapinduzi ccm Philemon Mollel maarufu kwa jina naMonaban akimwaga sera zake katika uzinduzi huo ambapo alikiri kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo endapo ataibuka mshindi katika uchaguzi mkuu
SAM_5742Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi akiongea katika mkutano huo
SAM_5804Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera Mahusiano na Uratibu Dkt.Mary Nagu akisalimiana na wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za CCM jimbo la Arusha mjini tarehe 5/9/2015 katika eneo la soko kuu jijini Arusha
SAM_5779Mjumbe wa halmashauri kuu  ya CCM Taifa kutoka Arusha mjini, Godfrey Mwalusamba akiongea katika uzinduzi huo
SAM_5786Mbunge viti maalum kundi la wanawake (UWT)Catherine Magige Mkoa wa Arusha akizungumza katika uzinduzi huo
SAM_5783Mbunge viti maalum na Kada maarafu kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Violet Mfuko akiongea katika uzinduzi huo
SAM_5771Aliyekuwa dereva wa Mbunge Lema shubet akiongea jukwaani alisema hamuogopi lema kwa kuwa mbinu zake zote anazijua hivyo hawezi hata kuua mende nyumbani kwakwe licha ya kumtangazia atamtumia majambazi nyumbani kwakwe
SAM_5793Mwigizaji maarufu wa sauti za viongozi mbalimbali Oscar Nyerere akichekesha katika uzinduzi huo
SAM_5787Mbunge mstaafu kupitia CCM jimbo la Longido Lekule Laizer  maarufu kwa jina la "kiboko wa wapinzani" akiongea katika uzinduzi huo ,aliwataka wananchi wa Arusha kumchagua Monaban kwakuwa ni kiongozi muadilifu mwenye sifa ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo
SAM_5812Mh.Phidesia Mwakitalima kulia anasema CCM mbele kwa mbeleeeeeeeeee!
SAM_5749Meza kuu
SAM_5807Mwenye miwani aliyekaa chini pamoja na wananchi Mustafa Panju ambaye alikuwa mgombea wa Ubunge kupitia CCM katika kura za maoni akifwatilia uzinduzi huo
SAM_5838Mustafa Panju ambaye alikuwa mgombea wa Ubunge kupitia CCM katika kura za maoni akiagana na wananchi baada ya kumaliza kampeni hizo

No comments:

Post a Comment