Saturday, July 11, 2015

TASWIRA MBALIMBALI KUTOKA KWENYE MKUTANO MKUU WA CCM MJINI DODOMA USIKU HUU

 Meza Kuu ikiongowa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete tayari kwa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi unaoendelea usiku huu kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM wa Dodoma Convition Centre, uliopo njia ya Kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, Mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Aliekuwa Mgombea Urais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM wa Dodoma Convition Centre, uliopo njia ya Kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, Mjini Dodoma.
 Baadhi ya Wake wa Viongozi wakiwa kwenye Mkutano huo.
 Mmoja wa Wagombea Urais alieingia kwenye hatua ya tatu bora, Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahaman Kinana akizungumza jambo na Aliekuwa Mgombea Urais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Dodoma Convition Centre, uliopo njia ya Kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, Mjini Dodoma.
 Mmoja wa Wagombea Urais alieingia kwenye hatua ya tatu bora, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya Mabalozi walioalikwa kwenye Mkutano huo.















No comments:

Post a Comment