Thursday, July 9, 2015

RAIS KIKWETE AFUNGUA UKUMBI MPYA WA MIKUTANO WA CCM, MJINI DODOMA LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza wakati wa wakati wa hafla ya ufunguzi wa Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, uliopo njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, mjini Dodoma leo Julai 9, 2015.Kulia kwake ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal na kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara, Mzee Phillip Mangula. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akibonyeza kitufe cha kengere kuashiria ufunguzi rasmi wa Ukumbi mpya na wakisasa wa mikutano wa CCM unaofahamika kwa jina la Dodoma Convention Centre, uliopo njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, mjini Dodoma leo Julai 9, 2015.Kulia kwake ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara, Mzee Phillip Mangula (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana pamoja na Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing wakifunua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Ukumbi mpya na wakisasa wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, uliopo njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, mjini Dodoma leo Julai 9, 2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Kikwete, akimkabidhi mfano wa ufunguo wa Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana, baada ya kuufungua rasmi ukumbi huo leo Julai 9, 2015 mjini Dodoma.
Picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali baada ya uzinduzi huo.



















1 comment: