Makamu wa Rais wa zamani wa Benki ya Dunia, Prof. Justin Yifu Lin akitoa mada yake juu ya uwanzishaji wa viwanda nchini Tanzania katika muadhara ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje |
Balozi Simba akichangia mada katika muadhara uliokuwa ukiendelea. |
Muhadhiri Chuo cha Diplomasia Bw. Innocent Shoo akiuliza swali. |
Afisa Mambo ya Nje Bi. Felisita Rugambwa naye akiuliza swali katika muhadhara.
|
Picha ya juu na chini ni watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje nao wakisikiliza mada kwa makini. |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akizungumza jambo huku akisikilizwa na Prof. Lin (Kulia) na Mhe. Membe (Katikati). |
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Diaspora Bi. Rosemary Jairo akizungumza jambo kwa Prof. Lin (kushoto) na Katibu Mkuu Balozi Mulamula. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K.
Membe, amesema upatikanaji wa gesi ni nyenzo muhimu ya uendelezaji wa
viwanda vya kati ili kutengeneza ajira na kuharakisha maendeleo ya nchi.
Mhe.
Membe alipongeza uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China
kuichagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tatu za Afrika itakapohamishia
baadhi ya viwanda vyake, akazitaka taasisi za uwekezaji na uendelezaji
wa viwanda kuweka mikakati madhubuti ya kutumia fursa hiyo kikamilifu.
Mhe.
Waziri alisema hayo leo wakati wa mhadhara wa aliyekuwa Mchumi Mkuu na
Makamu wa Rais Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Prof. Justin Yifu Lin,
kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar Es
Salaam, uliohudhuriwa na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na wadau
wengine.
Alisema
uendelezaji wa viwanda lazima utiliwe mkazo katika mpango wa Tanzania
kuingia uchumi wa kati 2025. "Tuache kukimbilia viwanda vikubwa
vinavyohitaji mitaji mikubwa, ambayo hatuna.
Tuchague viwanda vya kati vitakavyoajiri watu wengi kwa uwekezaji wa wastani."
Tuchague viwanda vya kati vitakavyoajiri watu wengi kwa uwekezaji wa wastani."
Mhe.
Membe alisema uendelezaji wa viwanda usambae nchi nzima ili kuvutia
vijana kuishi vijijini badala ya kukimbilia mijini. "Sasa hivi nchi yetu
ina viwanda takriban 3,000 lakini zaidi ya theluthi mbili viko Dar Es
Salaam. Lazima umeme upelekwe vijijini kuleta uwiano wa maendeleo ya
viwanda," alisisitiza.
Katika
mhadhara wake, Prof. Lin alisema nchi nyingi zinazoendelea zilifanya
maamuzi yasiyo sahihi kuhusu viwanda. "Nchi nyingi zilifuata kile
kinachoitwa Muafaka wa Washington na kuanzisha viwanda vikubwa kwa
maelekezo ya nchi tajiri, ambavyo viliwashinda kuendesha kwa kuwa
vilihitaji uwekezaji mkubwa sana."
Alisema
nchi za Asia zilizoendelea kwa haraka ni zile zilizoamua kuzingatia
mazingira halisi na kwenda hatua kwa hatua katika kuanzisha viwanda.
"Hii iliimarisha uchumi wao na kuukuza."
Prof.
Lin alisema serikali zina wajibu wa kusimamia uendelezaji wa viwanda
kwa kuweka sera sahihi, kuhimiza uwekezaji kwenye uzalishaji wa bidhaa
zenye masoko ya uhakika na kusaidia sekta binafsi ishiriki kikamilifu.
Akiongelea
Tanzania, Mchumi huyo wa Kichina alisema ingawa gharama za ajira ziko
chini, gharama za uendeshaji ziko juu, hivyo hazivutii uwekezaji.
Alisema moja ya sababu kubwa za Shilingi ya Tanzania kushuka thamani ni
uuzaji mdogo wa bidhaa nchi za nje.
No comments:
Post a Comment