Sunday, July 19, 2015

ALIYEKUWA MGOMBEA URAIS BALOZI MAHIGA AJITOSA UBUNGE IRINGA MJINI KUPITIA CCM

 Katibu  msaidizi  wa CCM Iringa mjini akipokea  fomu ya balozi Augustino Mahiga  anayeomba  kugombea  ubunge jimbo la Iringa mjini leo
 Balozi Mahiga  akirejesha  fomu  za  ubunge  jimbo la Iringa mjini leo


 Balozi  Mahiga  akiweka  sahihi  kitabu cha  wageni  leo
 Na  Matukiodaima BLOG

ALIYEKUWA  mmoja kati ya  wagombea zaidi ya 40 wa wagombea wa nafasi ya  urais Balozi mstaafu Augustino Mahiga amejitokeza  kuchukua na kurejesha fomu  wa  ubunge jimbo la Iringa mjini  kupitia chama  cha mapinduzi (CCM) huku akijihakikishia  kuwa  ndie anayestahili kumpokea  ubunge aliyemaliza muda  wake mchungaji Peter Msigwa (Chadema)

Balozi  Mahiga alieleza  kuwa yeye baada ya kustaafu nafasi ya ubalozi moja kati ya ndoto yake ni  kuendelea  kuwatumikia wananchi kwa ngazi ya  ubunge ama  udiwani kazi ambayo anaamini ataifanya kwa uadilifu mkubwa kama alivyofanya katika nafasi ya ubalozi wa Tanzania katika nchi  mbali mbali .

Akizungumza  leo  na  wanahabari  baada ya  kurejesha  fomu hiyo ya  ubunge katika  jimbo la Iringa mjini Balozi Mahiga  alisema  kuwa sababu kubwa ya chama  kupoteza umaarufu  wake ni makundi na  rushwa kwa baadhi ya  wagombea na  kuwa ni vema  wana CCM kuvunja makundi ya waliokuwa  wagombea wa nafasi za  urais ili kuepuka  kuingiza makundi hayo katika nafasi za ubunge na udiwani .

Kwani  alisema kwa  upande  wake haungi mkono baadhi ya  wana CCM kuendesha makundi na kuwa ndoto  yake ni  kuwatumikia  wananchi  hivyo baada ya  safari yake ya kutaka  kuomba  ridhaa ya  wana CCM kugombea Urais  kushindikana kwa  sasa atamuunga mkono kwa nguvu zote  mgombea wa CCM Dr John Mkagufuli na kuwa yeye ameamua  kugombea  ubunge japo alikuwa tayari hata kuwatumikia wananchi kwa nafasi yoyote ukiwemo udiwani .

Alisema  kipaumbele  chake  kikubwa ni  kusimamia na  kutekeleza kwa makini ilani ya CCM na  kuwa tofauti yake na aliyekuwa mbunge wa  jimbo la Iringa mjini kupitia chadema ni  moja kwani yeye ni mtendaji kwa vitendo zaidi na sio maneno pekee .

Kwani  alisema  kawaida  ubunge ni  kupokezana na kuwa Chadema  walipokea  jimbo  hilo  kutoka mikononi mwa CCM hivyo lazima Chadema kupokelewa jimbo  na CCM na mtu pekee anayestahili kuwatumikia wana Iringa ni  yeye pekee.

Alisema Iringa kama kitovu  cha utalii kwa mikoa ya nyanda za juu kusini anaamini iwapo chama kitamteua na kuwa mbunge wa  jimbo  hilo atahakikisha sekta  hiyo  inawanufaisha  wananchi  wake zaidi ikiwa ni pamoja na kuboresha makazi na nyumba kwa  kuweka mkakati kamili  wa  kufanya  hivyo.

Aidha  alisema  kuwa dhana ya  kutumia  pesa  ili  kupata nafasi ya  uongozi kama  ilivyokuwa kwa wagombea  Urais  inaweza  kuendeleza  kugawa  CCM na  kuwa utaratibu wa CCM wa  kuwatembeza  wagombea katika chombo  kimoja  cha  usafiri  utasaidia  kupunguza makundi ndani ya  chama  hicho na  kuwaonya watia nia wenzake  kuheshimu matokeo baada ya  mgombea kuteuliwa na  kuungana nae ili  kumnadi yule aliyepitishwa na chama .

Katika  jimbo la Iringa  mjini  hadi  leo majira ya saa 10  juioni jumla ya  wagombea 13  waliochukua fomu  waliweza  kurejesha  fomu  .

No comments:

Post a Comment