Mwenyekiti
wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Arusha na Mbunge wa Africa Mashariki
Mh.Bernard Murunya amabye alikuwa mgeni rasmi katika tukio la kukabidhi
pikipiki,akimkabidhi moja ya Pikipiki kwa katibu jumuiya ya wazazi
Wilaya ya
Arusha Rehema Mohamed jana katika makao makuu ya chama hicho jijini
Arusha, jumla ya pikipiki saba zilikabidhiwa kwa Wilaya saba katika Mkoa
wa Arusha huku Mwenyekiti wa Taifa Abdalah Bulembo pamoja Baraza kuu
Taifa wakifanya jitihada za kupatikana kwa Pikipiki hizo,katikati ni
Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau.(Picha na Pamela
Mollel wa jamiiblog)
Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau
akisoma risala fupi kwa mgeni rasmi ambapo katika risala yake alisema
kuwa ugawanyi wa pikipiki hizo saba ni juhudi za Mwenyekiti Taifa
Abdalah Bulembo pamoja na Baraza Kuu la Wazazi Taifa ,Tukio hilo ni la
Jumuiya ya wazazi Nchi nzima la kuwakabidhi Makatibu wa Wilaya zote 161
pikipiki kwaajili ya kurahisisha utendaji wa kazi na kuboresha suala
zima la usafiri ikiwa ni kuimarisha Chama cha Jumuiya zote
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Arusha na Mbunge wa Africa Mashariki Mh.Bernard Murunya akijaribu moja ya pikipiki alizokabidhi
No comments:
Post a Comment