Sunday, July 19, 2015

MUSTAFA PANJU ACHUKUA NA KURUDISHA FOMU YA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA ARUSHA MJINI AAHIDI UMOJA NA MAENDELEO

SAM_3880
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa Panju ambaye ni mmoja wa wagombea wa jimbo la Arusha mjini kupitia chama cha mapinduzi CCM akimkabidhi Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano fomu ya kuwania kinyang'anyiro hicho baada ya kuchukua fomu hiyo jana na kurejesha huku akisisitiza kuwa endapo atafanikiwa kupitishwa na chama hicho au laa atashirikiana na wananchi pamoja na wanaCCM katika kuleta maendeleo katika jimbo hilo ambalo lipo mikononi mwa chama cha Demokrasia na maendeleo( CHADEMA)Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_3827
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa Panju ambaye ni mmoja wa wagombea wa jimbo la Arusha mjini kupitia chama cha mapinduzi CCM akionyesha fomu ya kuwania nafasi ya ubunge baada ya kukabidhiwa na Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano jana katika ofisi za CCM wilaya
SAM_3886
Mustafa Panju akiandika jina lake katika fomu yenye majina ya waliokuja kuchukua fomu kupitia chama hicho kwa  Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano ,kushoto ni mke wake aliyemsindikiza kuchukua fomu
SAM_3889 
Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano akionyesha kadi ya mgombea ubunge kupitia chama cha CCM Mustafa Panju
SAM_3893 
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa Panju ambaye ni mmoja wa wagombea wa jimbo la Arusha mjini kupitia chama cha mapinduzi CCM akishikana mikono na kamati yake ya ushindi kulia ni Kassim Mamboleo  katibu wa kamati ya ushindi pamoja na mwenyekiti wa kamati hiyo
SAM_3834
Kassim Mamboleo ambaye ni katibu wa kamati ya ushindi ya mgombea Mustafa Panju akiteta jambo na Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano
SAM_3876
Mustafa Panju akiingia katika eneo la CCM wilaya huku akinyoosha mkono juu kusalimiana na wanaCCM baada ya kukamilisha taratibu za kujaza fomu yake ya kuwania ubunge jimbo la Arusha mjini
SAM_3830
Mgombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM Mustafa Panju akiongea na vyombo vya habari kuhusu nia yake ya kutaka kuliongoza jimbo hilo
SAM_3890
Picha ya pamoja na wadau,familia waliomsindikiza kuchukua fomu ya kuwania ubunge jimbo la Arusha mjini
SAM_3833 
Mustafa Panju akipiga picha na mmoja wa viongozi wa chama hicho kulia ni mke wake
SAM_3837
Timu ya Mustafa Panju ikiondoka eneo la CCM wilaya baada ya kumaliza taratibu zote za kujaza fomu na kurudisha

No comments:

Post a Comment