Sunday, July 19, 2015

Mh Godfrey Mgimwa Arudisha Fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa Kipindi kingine

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Iringa akipitia kadi ya uanachama wa Mgombea Godrey Mgimwa
Mh Godfrey Mgimwa (kulia) akikabidhi fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Kalenga baada ya kuijaza

Mbunge wa Jimbo la Kalenga Mh Godfrey Mgimwa Hii leo amerudisha fomu za kugombea Ubunge wa Jimbo hilo kwa kipindi kipya cha miaka mitano ijayo baada ya kuongoza jimbo hilo kwa muda wa Mwaka mmoja na Nusu tangu alipofariki aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo.
Mh Mgimwa amesema anajivunia mafanikio aliyoyapata katika kipindi hicho alicho kuwepo madarakani katika kuwaongoza wananchi wa Jimbo la Kalenga na kusema kuwa alipoingia madarakani alikutana na changamoto lukuki zilizokuwa zikiwakabili wananchi wake hivyo tayari baadhi ya changamoto tayari amekwisha zishughulikia na zingine anaendelea kuzitatua
"nimezikuta changamoto kadhaa zilizokuwa zikiwakabili wananchi lakini mpaka leo tayari kuna baadhi tumezimaliza na zingine tunaendelea kuzikabili na tutazimaliza hivyo ninagombea ili niweze kuwafikisha wananchi wa jimbo la kalenga pale wanapo pataka" alisema Mgimwa
Aidha Mh Mgimwa alisema katika kipindi chake cha uongozi amejitahidi zaidi kusukuma mbele jitihada za wananchi za kujiletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kuinua vikundi mbalimbali vya wajasiliamali,kuchangia katika shughuli za ujenzi wa maabara,uhamasishaji wa nishati na huduma za Afya hivyo alisema kazi hiyo itaendelea katika kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.
"katika kipindi kijacho ninamini nitafanya zaidi kwa kuwa kitakuwa ni kipindi kirefu na ninaamini utakuwa ni wakati mzuri wa kukamilisha yale yote makubwa tuliyoyaanza kwani kwa kipindi hiki kifupi baadhi ya changamoto tumezitatu pia hiki kinachofuata kitakuwa ndicho kipindi ambacho nitashughulikia kero za moja kwa moja zinazo wakabili wananchi kwani zile za jumla tutazimaliza mapema" alisema
Mgimwa amerudisha fomu hiyo hii leo akiwa ni miongoni mwa makaada watano wa Chama Cha Mapinduzi kuchukua fomu za kuwania kugombea Ubunge katika jimbo Hilo la Kalenga. 

No comments:

Post a Comment