Monday, July 6, 2015

MTIA NIA WA NAFASI YA UBUNGE MOSHI VIJIJINI ,EVARIST KIWIA AJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUPIGIA KURA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi vijini Evarsit Kiwia akitoa maelezo binafsi mbele ya afisa wa tume alipofika kujiandikisha kupitia mfumo mpya wa BVR katika kata ya Old Moshi Magharibi.
Kiwia akijaza moja ya fomu zinazotakiwa kujazwa wakati wa zoezi a uandikishwaji.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge jimbo la Moshi Vijijini ,Evarist Kiwia akichukuliwa Taswira kwa ajili ya kupatiwa kitambulisho maalumu kwa ajili ya kupigia kura.
Kiwia akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kupitia mfumo mpya wa BVR.
Na Dixon Busagaga WA globu ya jamii Kanda ya Kaskazini,Moshi.

CHAMA cha Demkrasia na Maendeleo (Chadema) katika jimbo la Moshi vijini kimeonesha kuwa na hofu kwa baadhi ya wananchi kushindwa kuandikishwa katika zoezi la uandikishaji kwa kutumia mfumo mpya wa BVR huku kikiiomba tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) kuongeza muda wa zoezi la uandikishaji kwa wakazi wa maeneo hayo.

Ombi hilo limekuja kutoka na kuwepo kwa madai ya kuwa baadhi yam ashine hazikuweza kufanya kazi vizuri hali iliyolazimu baadhi ya wananchi kushindwa kujiandikisha.

Sababu nyingine iliyopelekea ombi hilo ni kuhusu jiografia ya jimbo hilo pamoja na shughuli ambazo zimekuwa zikifanywa na wakazi wa maeno hayo ambao wengi wao wamekuwa wakitumia muda mwingi kufanya kazi ya kilimo na ufugaji hali inayochangia kukosa muda wa kutoka kwenda kupanga foleni kwa ajili ya uandikishwaji.

Akizungumza mara baada ya kujiandikisha Menyekiti wa Chadema jimbo la Moshi vijijini ,Ekarist Kiwia alisema kutokana na usumbufu unaotokana na mashine za BVR ni vyema tume ikatizama namna ya kuongeza muda wa zoezi la uandikishaji.

“Mimi mwenyewe nimeshindwa kujiandikisha  katika kituo cha Mande Kanisani ambapo ndiko eneo la langu ….nimeenda kitongoji kingine nikapewa ridhaa ya kujiandikisha lakini wako watu wanakosa fursa ya kujiandikisha kutokana na mashine kutofanya kazi vizuri”alisema Kiwia.

Kiwia ambaye pia ni miongoni mwa watia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo kupitia Chadema ,alisema licha ya uwepo wa changamoto hizo wananchi hawana budi kujitokeza kwa wingi ili kupata kitamburisho cha kupigia kura kitakachosaidia kumpata kiongozi bora wa jimbo hilo.


Kwa upande wao wananchi wa  kata ya old Moshi Magharibi walisema wamehamosika kujitokeza katika zoezi la uandikishaji,isipikuwa changamoto za mashine za BVR ndio zimekuwa zikiwakatisha tamaa kuendelea kungojea katika foleni.


Elizabeth  Massawe na Alex Kiwia walisema  kuwa walitakiwa kufanya kijiandikisha katika kituo cha Mande kanisani lakini  kwa siku tatu maofisa katika kituo hicho wanadaiwa kuwajibu wananchi kuwa  mashine ni chafu za kusafisha na kwamba hawana uhakika wa kujiandikisha.

“Mimi hata nikienda kituo cha jirani hawakubali   kuniandikisha  wanasema nijiandikishie sehmu ninayoishii sehemu ninayokaa ndio hizo mashine hazifanyi kazi mara utaambiwa ni zakusafisha huku muda wameweka kidogo ni wiki moja tuu”alisema Massawe.

Kiwia alisema utaratibu uliowekwa na tume kuwa watu wajiandikishie shemu ambayo wanatoka  ni mbaya kutokanana kwamba mashine za BVR zinasumbua na hazitabiriki.

Alisema wananchi wengi watakosa haki yao ya msingi ya kupiga kura kutokana na kushindwa kujiandikisha na kwamba muda uliopangwa ukiisha wanondoka bila kuandikisha wananchi wote.

No comments:

Post a Comment