Friday, July 17, 2015

MGOMBEA UBUNGE VITI MAALUMU ARUSHA,NEEMA AAHIDI KUINUA VIJANA KIUCHUMI

SAM_3817
Katibu wa vijana umoja wa vijana  UVCCM wilaya ya Arusha mjini Jamali Khimji akimkabidhi fomu ya ubunge viti maalum Bi.Neema Kiusa(27)katika ofisi za umoja huo jijini Arusha, ahaidi kuinua vijana kiuchumi endapo atapata nafasi ya kuwa Mbunge wa vijana Mkoa wa Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_3820
Neema Kiusa(27) Mgombea ubunge viti maalumu kupitia  chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana wilaya ya Longido akionyesha fomu aliyochukua leo.
SAM_3821
Neema Kiusa(27)ambaye ni mgombea ubunge viti maalumu kupitia  chama cha Mapinduzi  akiwa na mumewe Andrea Shija, pia ni mama wa mtoto mmoja
SAM_3824
Neema Kiusa(27)Mgombea ubunge viti maalumu kupitia  chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana wilaya ya Longido akitoka katika ofisi za umoja wa vijana wa ccm mkoa wa Arusha baada ya kuchukua fomu 

Mgombea ubunge kupita kundi la vijana (UVCCM) Neema Kiusa  leo amechukua fomu ya kuwania nafasi ya ubunge viti maalumu Mkoa wa Arusha,ambapo amesema kuwa shauku yake kubwa ni kuwatumikia vijana kwa kutatua changamoto ya ajira 
Neema ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana Wilaya ya Longido alisema kuwa ndoto yake ya kuwatumikia vijana ni ndoto yake ya muda mrefu sana hivyo endapo atapata nafasi hiyo atashirikiana na vijana bega kwa bega kuleta maendeleo katika Mkoa wa Arushaa 
Pia mgombea huyo alitoa shukrani kwa mume wake  anayempa ushirikiano mkubwa wa kufanikisha ndoto yake ya kutumikia vijana ambapo aliwataka wanaume wengine kuonyesha ushirikiano kwa wake zao endapo wataonyesha nia ya kuwania nafasi za uongozi
Kwa upande wake Katibu wa vijana UVCCM wilaya ya Arusha mjini Jamali Khimji amewataka vijana wa chama cha mapinduzi kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za nafasi za ubunge viti maalumu kundi la vijana katika mkoa wa Arusha
Khimji alisema kuwa kijana anayetakiwa kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ni kijana wa kwanzia umri wa miaka 21-30 na awe ametimiza vigezo vya chama hicho

No comments:

Post a Comment