Saturday, July 25, 2015

LEMA KUPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA NA JOYCE MUKYA

SAM_4216Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akizungumza katika uchaguzi wa kumpata Mbunge pamoja na Mbunge viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA)jijini Arusha ambapo aliibuka kidedea kwa kura 255 sawa na asilimia 93.06% (Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_4210Mbunge viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joyce John Mukya alipata kura 39 sawa na asilimia 73.6% katika kinyang'anyiro hicho hivyo kumfanya kuwa Mbunge wa viti maalum,aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuvunja makundi ili kuhakikisha chama kinashinda katika uchaguzi wa Urais,Ubunge na udiwani 
SAM_4212 Mgombea kupitia chama cha Demokrasia na maendelao (CHADEMA)Noel Olevaroya akizungumza mara baada ya kutangazwa kushika nafasi ya pili  kwa kupata kura 13 sawa na asilimia 4.74% katika kinyang"anyiro hicho ambapo aliwashukuru wajumbe wa mkutano huo na kuhaidi kumpa Mbunge Lema shilingi laki tano kwaajili ya kampeni ya kuhakikisha  chama hicho kinapata ushindi wa kishindo
SAM_4147Wagombea ubunge viti maalum Mkoa wa Arusha wakisubiria kuingia kujinadi kwa wajumbe wa mkutano
SAM_4214Mgombea nafasi ya Ubunge,Nsajigwa Mwakatobe aliyepata kura 6 sawa asilimia 2.18% akiwashukuru wajumbe wa mkutano pamoja na wanachama wa chama hicho
SAM_4208PIPOOOOZ!Mgombea nafasi ya Ubunge viti maalum Grace Macha alipata kura 3 katika kinyang'anyiro hicho , akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo na kuhaidi kushirikiana nao 
SAM_4142Wajumbe wa mkutano huo
SAM_4195Taswira  katika mkutano huo
SAM_4207
Mgombea nafasi ya Ubunge viti maalum Glory Bernad akishukuru katika mkutano huo
SAM_4201Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akisaini fomu ya uchaguzi,pembeni ni Mbunge wa Rombo na mwenyekiti wa uchaguzi huo Joseph Selasini
SAM_4194Mbunge wa Rombo na mwenyekiti wa uchaguzi huo Joseph Selasini akitaja washindi katka kinyang'anyiro hicho
SAM_4198Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa na mtoto wake aliyemkimbilia mara baada ya baba yake kutangazwa mshindi katika uchaguzi huo
SAM_4222Wajumbe wakimshangilia Mbunge viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joyce John Mukya 
SAM_4196
SAM_4152

No comments:

Post a Comment