Tuesday, October 27, 2015

WILFRED LWAKATARE WA CHADEMA AIBUKA KIDEDEA UBUNGE BUKOBA MJINI

Hatimaye Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama cha demokrasia na maendeleo -Chadema Bw. Wilfred Lwakatare ameibuka kidedea leo hii kuwa Mbunge wa Bukoba Mjini akiibuka kidedea dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Kagasheki. Matokeo hayo yametanga usiku huu punde na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli. Kura za Udiwani Chadema/ Ukawa imeshinda Kata zifuatazo: Kahororo, Kagondo, Kibeta, Kitendaguro, Nshambya, Hamugebe, Kashai, Bakoba na Bilele. CCM imepata Kata ya Rwamishenye, Buhembe, Miembeni, Nyanga na Ijunganyondo. 

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli akitoa matokeo usiku wa kuamkia leo saa 2:30 na kumtangaza Lwakatare kwamba ndie mshindi na Nafasi hiyo ya Ubunge Bukoba Mjini. 
Bw. Aron T. Kagurumjuli(Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini) akiendelea na zoezi la kutangaza matokeo usiku huu.
Mshindi wa nafasi ya Ubunge wa Bukoba Mjini Bw. Wilfred Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA akifurahia baada ya kuibuka kidedea katika kinyang'anyiro hicho baada ya kumwangusha mgombea mwenza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Sued Kagasheki usiku huu. Picha na Faustine Ruta, Bukoba


Licha ya kuonekana kana kwamba hapakuwa na dalili zozote za fujo wakati wa zoezi la upigaji kura za Ubunge na udiwani, hali ilibadilika  jumatatu asubuhi baada ya wafuasi wa chama cha Chadema kutaka matokeo mapema baada ya kupata matokeo hayo usiku wa kuamkia leo hii kuwa Chadema imeshinda katika Kata 9 kati ya 14 wafuasi hao waliandamana katika maeneo ya mji wa Bukoba wakitaka majibu yatolewe mapema. Kitu ambacho hakikufanyika na Jioni hii kuleta kasheshe na ghasia. Hali hiyo ilisababisha polisi wa kutuliza ghasia kuingilia kati na kuwatawanya vijana hao ambao mpaka usiku  walikuwa wamepandwa na jazba katika eneo la ofisi za Halmashauri ya Bukoba. Vurugu zikiwemo kurushiana mawe zilitokea. Ndipo polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokusanyika katika Ofisi za Halmashauri na kuanza kurusha mawe wakishinikiza kutangazwa kwa matokeo ya ubunge. Hali hiyo ilitulia baada ya Viongozi wa Chadema kuwatuliza na ndipo Matokeo yakatangazwa. 
Taarifa zinasema kuwa kulikuwa na mchuano mkali kati ya wagombea hao wawili ambao ni Wilfred Lwakatare wa chama cha Chadema na aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia chama cha CCM Khamis Sued Kagasheki. Kitu kilichopelekea kurudiwa kuhesabiwa kwa kura zote na kupata uhakika wa kutosha.

Kura zilizokubalika ni 54,211 sawa na asilimia 98.54, kura zilizoharibika ni 805 sawa asilimia 1.46, Matokeo ni kama ifuatavyo TLP kura 81 sawa na asilimia 0.2, ACT kura 453, Khamis Sued Kagasheki wa CCM amepata kura 25,565 sawa na asilimia 47.2, Wilfred Lwakatare wa Chadema amepata kura 28,112 sawa na asilimia 51.9Wafuasi wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika katika Ofisi za Halmashauri Bukoba wakidai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa huo wa Wabunge.
Vingozi wa Chama cha Chadema wakiteta jambo, kushoto) ni Bw. Chief Kalumuna Mshindi wa Udiwani Kata ya Kahororo aliyeshinda kiti hicho katika Uchaguzi huu wa 2015. (Kulia) ni Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya Bukoba Victor Sherejei.
Bw. Wilfred Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Kahororo kupitia Chama cha Chadema katika Ofisi za Halmashauri ya Bukoba mjini huku wakisubiri matokeo ya Ubunge Bukoba Mjini.
Bw. Wilfred Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya Bukoba Victor Sherejei (kulia) mbele akiteta na Chief Kalumuna Diwani wa kata kahororo wakibadilisha mawazo wakati wakisubiri matokeo usiku huu.Waandishi wa habari na Makada wa Chama cha Chadema wakiwa katika Ofisi za Halmashauri ya Bukoba
Kidedea...Chif Kalumuna(kulia) wa Kata ya Kahororo akiwa amembeba mshindi bw. Wilfred Lwakatare
Wafuasi wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika kutaka kuvamia Ofisi za Halmashauri ya Bukoba kudai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa wabunge na Polisi walikuwa tayari kuwakabili vilivyo na kuzuia umati huo mkubwa.
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo yatolewa baada ya kuchukuwa muda tangu asubuhi mpaka jioni hii.
Taswira jioni hii maeneo ya karibu na Ofisi za Halmashauri.
Hapa ikabidi kiongozi wa Chadema aliyeshinda katika Kata ya Kashai kupitia chama hicho awatulize kwamba matokeo yanaenda kutolewa jioni hii.
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo ya Kiongozi wao.

No comments:

Post a Comment