Mjumbe wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi Ndg.Mwigulu Nchemba akiwasili Jimbo la Simanjiro na kupokelewa na Mbunge mtarajiwa wa Jimbo hilo Ndg.Ole Sendeka mapema hii leo.Mwigulu Nchemba akimnadi Ole sendeka kwa wananchi wake,Kubwa ni Ujasiri wa Ole sendeka kwenye kutetea maslahi ya taifa,Ufuatiliaji wa Miradi ya maendeleo kama barabara zinazokwenda kujengwa kwa kiwango cha rami kuunganisha na mikoa inayopakana na SImanjiro.Ole Sendeka akizungumza na Wananchi wake wa kata ya Engesbert kuhusu Ilani ya CCM na maendeleo ya Jimbo la SImanjiro.Kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi Jimbo la Simanjiro linakwenda kujengwa barabara za Rami Zaidi ya Tatu za kutoka Arusha,Mererani na Dodoma na ile ya Babati kwenda Simanjiro.
Mbali na hilo,Uboreshaji wa Mfumo wa majini na Uchimbaji wa Visima ndio kipaumbele cha kwanza kwa Ole sendeka kwa Wananchi wa Simanjiro.Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Namalulu Jimbo la Simanjiro.Twende na Magufuli popote alipo.Wananchi wa kata ya Namalulu wakionesha Umoja wao kuichagua CCM kwa nafasi za Udiwani,Ubunge na Urais katika Uchaguzi wa October 25 Mwaka huu.Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa kata ya Namalulu.Vijana wa Kimaasai "Molan" wakiwa njiani kuelekea kwenye Mkutano wa Mwigulu Nchemba kata ya Loibosoit.Mwigulu Nchem akiwasili kata ya Loibosoit kwaajili ya kumuombea Kura Rais ajaye wa awamu ya tano Ndg.J.Pombe Magufuli,Mbunge na Diwani wa Chama cha Mapinduzi.Wananchi wakiiitikia kuwa chaguo lao ni "kazi tu" wakimaanisha Magufuli kwa nafasi ya Urais.Wananchi wakimsikiliza Miwgulu Nchemba.wananchi wakichukua kumbukumbu za Mkutano wa hadhara wa Mwigulu NChemba wa kuinadi Ilani ya CCM.Mwigulu Nchemba akiondoka kata ya Loibosoit.Hatimaye Mwigulu Nchemba akawasili Jimbo la Kondoa Vijijini kata ya Kolo kuinadi ilani ya CCM.Wananchi wa kata ya Kolo wakishangiliwa ujumbe wa Mwigulu Nchemba kwao kuwa "CCM imeamua kumleta Magufuli kwenye Nafasi ya Urais ili Mafisadi na Walarushwa wakimuangalia waseme sasa rushwa basi,Lakini pia kwa wazembe waanze kujiandaa kutafuta kazi ya kufanya kama hawatabadilika kwenye serikali ya Magufuli"Mwigulu Nchemba akimnadi Diwani wa kata ya Mondo jimbo la Chemba Ndg.Sambala.Wananchi wa Mondo wakimsikiliza Mwigulu Nchemba kwa makini,Kuwa mabadiliko mazuri ya ya maendeleo sio vyama.Amewaomba wamchague Sambala aendelee na ujenzi wa kituo cha Afya cha kata ya Mondo,Lakini mradi wa maji mkubwa umeshaanza kufanya kazi.Mwigulu Nchemba akiondoka kata ya Mondo jioni ya leo.Mwigulu Nchemba akishangiliwa mara baada ya kuwasili kata ya Kibaya Jimbo la kiteto.Mwigulu "Nawaonya wote wanaofanya siasa zisizo za kistaarabu,Vyama vya siasa vipo kikatiba na Mikutano yake ipo kikatiba na Mavazi ya kila chama yapo kikatiba,Nawaombeni kama mkutano sio wa chama chako ila unapenda kwenda kusikiliza kinachozungumzwa jitahidi uwe mvumilivu,Ukianza kubishana na wenye mkutano unajitafutia matatizo"CCM imemleta Magufuli kwa malengo,Kama Taifa tunataka kukomesha swala la Rushwa,Kukomesha Utendaji wa kimazoea na Mbovu,Kukomesha Matapeli wanaotoa mbole na pembejeo mbovu kwa wakulima na wafugaji,Mtu sahihi anayeweza kushughulika na watu hao ni Magufuli tu.Nawaombeni mkamchague Magufuli kwa Maendeleo ya kweli ya taifa letu".Mamia ya Wananchi wa Kiteto kata ya Kibaya wakimsikiliza Comrade Mwigulu Nchemba jioni ya leo alipofika Kumnadi Mbunge mtarajiwa Ndg.Papian wa Chama cha Mapinduzi.Mkutano wa Mwisho kwa leo,Mwigulu Nchemba anamalizika kata ya Matui Jimbo la Kiteto.Anawasisitiza Wananchi kuunganisha nguvu zao kumpigia kura Magufuli kwa Urais,Ubunge na Udiwani pia uende kwa CCM.Ilani inayotekelezeka kwa Jimbo la Kiteto na Nchi nzima ni ya chama cha Mapinduzi. Picha na Sanga Festo Jr.
No comments:
Post a Comment