Thursday, October 1, 2015

BI. SAMIA SULUHU AAIDI NEEMA KWA WAKAZI WA MUSOMA MKUTANO WA KAMPENI...!

Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwasenge, Jimbo la Musoma Mjini. Katika hotuba yake aliwaomba wanaMusoma kuichagua CCM ili iweze kuunda Serikali kwani imepanga kuboresha huduma mbalimbali za kijamii pamoja na ujenzi wa miundombinu eneo hilo itakayochangia kukua kwa biashara anuai.
 Alisema Serikali itakayoundwa na CCM imepanga kujenga maeneo ya kisasa ya maegesho ya meli (magati) Musoma na ndani ya miezi mitatu huduma ya maji maeneo mbalimbali itapatikana kwa uhakika kutokana na kukamilika kwa mradi wa maji eneo hilo. Aliongeza pia ili kuboresha huduma za Mwisenge zahanati ya eneo hilo itabadilishwa mara moja na kuwa kituo cha afya.
Kulia ni baadhi ya wasanii maharufu wa uigizaji wakishangilia wakati Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Mwisenge.

Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Sirari wakifikisha ujumbe wao kwa Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipohutubia wananchi katika viwanja vya Tarafa Sirari.

Sehemu ya wanaCCM na wananchi wakimshangilia  Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia Mwisenge, Musoma Mjini.

Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime, Rashid Bugomba alipowasili Sirari kwa mkutano wa kampeni kuinadi CCM eneo hilo..

Wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia wananchi Kata ya Sirari
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwatambulisha baadhi ya wagombea ubunge wa Wilaya ya Tarime kwenye Mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Sirari.

Ni mwendo wa 'PUSH UP' baadhi ya wananchi wakipiga 'Push Up' kwenye mkutano wa mgombea mwenza Sirari kuonesha kuwa wapo 'fit'.
Sehemu ya wanaCCM na wananchi wakimshangilia  Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia Mwisenge, Musoma Mjini.
Sehemu ya wanaCCM na wananchi wakimshangilia  Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia Mwisenge, Musoma Mjini.
Wananchi wakisikiliza hotuba ya baadhi ya viongozi wa CCM Wilaya ya Musoma.

Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM Viwanja vya Mwisenge.

Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM Viwanja vya Mwisenge.

Aliyekuwa mbunge wa CCM, Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza na wananchi katika viwanja vya Mwisenge.

Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie na wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM Viwanja vya Mwisenge.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com

No comments:

Post a Comment