Tuesday, October 13, 2015

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KIBAHA MJINI AHAIDI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO YA AJIRA KWA VIJANA

Mgombea ubunge wa jimbo la kibaha mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM)    Silvestry Koka akiwahutubia wananchi wa kata kongowe pamoja na boko timiza katika moja ya mkikutano yake ya hadhara.
Mgombea ubunge kupitia CCM jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akiwa anawasali  na kupokelewa kwa shangwee  katika uwanja kabla ya kuanza kuwahutubia wawananhci walijitokeza na kufurika kwa wingi kusikiliza sera za mgombea huyo.
Umati wa waanachi pamoja na wanahama wa chama cha mapinduzi wakiwa wamefurika kwa ajili ya kumlaki mgombea huyo hayupo pichani wakati alipokuwa akiwasili katika kuwahutubia wananachi katika mkutano huo wa hadhara.
moja ya kikundi cha sanaa kutoka Wilayani Kibaha kikionyesha mbwembwe na manjonjo ya ina yake  ya  kwa wananachi waliofika kwa wingi kucheza katika moja ya mikutano hiyo ya mgombea ubunge jimbo la Kibaha mjini.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini akiwa anawasili katika mkutano mwingine ambao ulifanyika katika kata ya visiga huku akiwa na walinzi wake ambao wanahakikishia usalama na utulivu unakuwepo katika kila sehemu.
 Mgombea huyo akiwa anapandisha bendera kwa ajili ya kuashilia ufunguzi wa tawi la wakeleketwa katika kata ya visiga(Picha zote na Victor Masangu)

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka amesema kwamba endapo akichaguliwa tena na wanachi wanachi ndoto yake kubwa ni kuwasaidia vijana kwa hali na mali katika upatikanaji wa fursa za ajira sambamba na kuwawezesha mitaji katika vikundi vyao  vya ujasilimari ili waweze kujiajiri wao wenyewe. na kuleta mabadiliko chanya katika kukuza uchumi.

Ahadi hiyo imetolewa na Mgombea ubunge Jimbo la Kibaha mjini Silivestry Koka wakati wa mkutano mikutano yake  ya  hadhara ya kampeni wakati akizungumza na wananchi wa maeneo mbali mbali mtaa wa boko  timiza  pamoja na kata ya  Kongowe ambapo alisema kuwa lengo kubwa ni kuwainua vijana wasiwe tegemezi.

Koka alisema kwamba anatambua vijana wengi wa katika jimbo la kibaha mjini wana ujuzi katika fani mbali mbali hivyo atahakikisha anaweka mpango mkakati katika uongozi wake ambao utaweza kuleta mabadiliko  ya kuwapatia fursa za ajira vijana hao kupitia baadhi ya  viwanda vilivyojengwa pamoja na kuendelewa kuwainua kwa njia za kuwaongezea mitaji.

“Kitu kikubwa wananchi wa jimbo la kibaha ninawaomba mnichague katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, na mimi nitahakikisha ninapambana kwa kw audi na uvumba ii kuweza kuhakikisha kwamba vijana kupitia makundi yao ya ujasiriamali pamoja na wale ambao hawana vikundi ninawaunganisha kwa pamoja na kuwasaidia mitaji ili waweze kujiendeleza zaidi katika shughuli za ujasiliamali,”

“Mbali na kuziwezesha vikundi  vijana mkao mkao wa kula kwani kwa sasa kuna viwanda katika jimbo la Kibaha mjini hivyo fursa hivyo ipo na nitakuwa nanyi bega kwa bega kuwatafutia ajira katika maeneo mbalimbali na nina imani jambo hilo linawezekana na mimi nitalisimamia mwanzo hadi mwisho ili nione vijna wote wanajishughulisha na kazi na sio kukaa bila ya kujituma,”alismea Koka.

Aidha alisema kwamba sehemu zote hata nchi za nchi maendeleoa yanakuja kwa kasi endepo kukawa na mpango  endelevu na madhubuti wa kuwawezesha vijana katika soko la ajira ambalo ndilo mkombozi mkubwa katika kukuza uchumi na kupambana na janga la umasikini.

Mgombea huyo katika hatua nyingine aliwahakikishsia wananchi kulisimamia kwa ukaribu  suala la changamoto ya uhaba wa madawa katika zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali kwani limekuwa ni kero kubwa ya siku nyingi kwa waanahci wanapokwenda kupatiwa matibabu dawa wanakosa na wanahitajika kwenda kununua sehemu nyingine hali  ambayo amedai hawezi kuifumbia macho.

Kwa upande wake mwanachi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Japhari alisema kwamba kwa sasa pindi wanapokwenda kutibiwa wanapata usumbufu mkubwa sana kwani pamoja na kutozwa fedha ya kumwona dakatari lakini bado kuna tatizo la upatikanaji wa madawa hivyo kiongozi atakayepata nafasi ya kuchaguliwe aliangalia suala hilo kwa macho  matatu ili kuweza kuboresha huduma ya afya.

No comments:

Post a Comment