Saturday, August 1, 2015

LOWASSA ARUDISHA FOMU ZA KUWANIA URAIS KUPITIA CHADEMA, ADHAMINIWA NA ZAIDI YA WANANZANIA ZAIDI YA MIL. 1.6

 Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiwapungia maelfu ya wafuasi na wapenzi wa Chama hicho, wakati alipowasili kwenye Ofisi ya Makao Makuu ya Chama hicho, Kinondoni Jijini Dar es Salaam jioni ya leo. Mh. Lowassa alifika ofisini hapo kurudisha fomu za kuomba ridhaa ya Chama hicho, kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.Kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Mh. Godluck Ole Medeye alieambatana nae.
 Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA - Zanzibar, Salum Mwalim wakati akilakiwa kwenye Makao Makuu ya Chama hicho, Kinondoni Jijini Dar es salaam leo.
 Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wafuasi wa Chama hiyo kwa ishara ya vidole viwili.
 Sehemu ya Viongozi wa CHADEMA waliokuwepo kwenye hafla hiyo.
 Baadhi ya Wadau walioambatana na Mh. Lowassa.
 Wakitambulishwa.
 Mkurugeni wa Oganaizesheni na Uratibu wa Kanda wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Benson Kigaila akionyesha fomu zenye idadi ya wananchi waliomdhani Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama hicho, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa. ambapo jumla ya wananchi 1,662,397 walijitokea katika maeneo mbali mbali kumdhamini Mgombea huyo.
 Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa (wa pili kulia) akikabidhi fomu hizo kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Prof. Abdalaah Safari wakati wa hafla fupi ya kurudisha fomu hizo, iliyofanyika jioni ya leo kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA, Kinondoni Jijini Dar es salaam. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Wadhamini wa CHADEMA, Mh. Arcado Ntagazwa na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA - Zanzibar, Salum Mwalim.
Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Prof. Abdalaah Safari wakionyesha fomu hizo kwa wanahabari.Kushoto ni  Mwenyekiti wa Wadhamini wa CHADEMA, Mh. Arcado Ntagazwa.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Prof. Abdalaah Safari akizipitia fomu hizo.
Mwanasheria wa CHADEMA, Mh. Mabere Marando akizipitia fomu hizo kama zimejazwa sawa sawa.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Prof. Abdalaah Safari akizungumza machache baada ya kupokea fomu hizo.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Prof. Abdalaah Safari akipongezwa na Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa.
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA - Zanzibar, Salum Mwalim akizungumza.
Sehemu ya Wabunge wa CHADEMA waliokuwepo.






No comments:

Post a Comment