Monday, August 31, 2015

DKT. SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM CCM ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa CCM wakati alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Uguja kuhudhuria katika Kikao cha Siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanzibar kilichofanyika leo katika ukumbi Ofisi hiyo Mjini Unguja.
Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanzibar wakipitia makabrasha ya kikao hicho kabla ya kuanza leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
Wajumbe wa Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanzibar wakipitia makabrasha yenye agenda za kikao kabla ya kuanza hicho leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanzibar wakimkaribisha kwa makofi na kuimba wimbo wa Chama wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,alipoingia katika ukumbi wa Kikao hicho kilichofanyika leo Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai wakiimba Wimbo wa Chama cha Mapinduzi kabla ya kuanza kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanzibarkilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai kabla ya kuanza kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanzibar kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
Wajumbe wa Sekteratieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanzibar wakiwa katika kikao cha Siku moja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akitoa taarifa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanzibar kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiendesha kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanzibar kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai.
Wajumbe wa Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanzibar wakimsikiliza Mwenyekiti wa kikao Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.[Picha na Ikulu.]

KAMATI Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi imekutana leo, chini ya Mwenyekiti wake Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya Organaizesheni kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, imesema kikao hicho cha kawaida kilifanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Mjini Zanzibar.

Taarifa imesema kikao pamoja na mambo mengine, kimewataka  Viongozi,  Watendaji na Wanachama wa CCM wa ngazi zote kufanya kazi kuhakikisha wagombea  wote  wa Chama hicho hasa wa Viti  vya Urais wa Zanzibar  Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli wanashinda kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

Kikao pia kimewataka Viongozi wa CCM wa ngazi zote  kuendeleza na kuimarisha mshikamano miongoni mwao hususan  wakati huu wa kuelekea kwenye kampeni na uchaguzi mkuu, ili ushindi uweze kupatikana.

Hadi sasa Chama Cha Mapinduzi kimesimamisha wagombea wake katika Majimbo yote 50 kwa nafasi ya Ubunge na 54 kwa nafasi ya Uwakilishi Visiwanni Zanzibar. Aidha, kimesimamisha  wagombea wake katika Wadi zote Unguja na Pemba.

Kikao pia kimeunda  Kamati  Kamati Ndogo ya Kampeni  yenye Wajumbe ishirini (20) itakayoongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Katibu wake  ni  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe. Vuai Ali Vuai.

Wajumbe hao ni pamoja na :-
1.    Mhe. Balozi Seif Ali Iddi                      -           Mwenyekiti
2.    Mhe. Vuai Ali Vuai                              -           Katibu
3.    Mhe. Shamsi Vuai Nahodha              -           Mjumbe
4.    Mhe. Haji Mkema Haji                                    -           Mjumbe
5.    Mhe. Hamad Yussuf Masauni           -           Mjumbe
6.    Mhe.    Waride Bakari Jabu                -           Mjumbe
7.    Mhe. Seif Shaaban Mohamed            -           Mjumbe
8.    Mhe. Najma Murtaza Giga                 -           Mjumbe
9.    Mhe. Dkt. Maua Abeid Daftari            -           Mjumbe
10.  Mhe.    Prof. Makame M. Mbarawa   -           Mjumbe
11.  Mhe. Omar Yussuf Mzee                   -           Mjumbe
12.  Mhe. Ramadhan A. Shaaban             -           Mjumbe
13.  Mhe. Mohamed A. Mohamed                        -           Mjumbe
14.  Mhe. Khadija Hassan Aboud              -           Mjumbe
15.  Mhe. Haroun Ali Suleiman                  -           Mjumbe
16.  Mhe. Issa Haji Ussi Gavu                  -           Mjumbe
17.  Mhe. Mahmoud Thabit Kombo           -           Mjumbe
18.  Mhe.    Shaka Hamdu Shaka             -           Mjumbe
19.  Mhe. Balozi Ali Abeid Karume            -           Mjumbe
20.  Mwakilishi kutoka UWT                      -           Mjumbe.

Mwisho.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI




Sgd.
(Haji Mkema Haji),
Katibu Kamati Maalum ya NEC,
Idara ya Organaizesheni - CCM
ZANZIBAR.

30 Agosti, 2015.

No comments:

Post a Comment