Tuesday, September 29, 2015

MSAFARA WA LOWASSA WASIMAMISHWA ZAIDI YA MARA NNE WAKATI AKIWA SAFARINI KUTOKEA JIJINI TANGA KUELEKA DAR

 Msafara wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, ukichanja mbuga kutokea jijini Tanga kuelekea jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi.
Sehemu ya wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, wakiwa wamefunga barabara, wakimtaka Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, azungumze nao leo Septemba 29, 2015, wakati akiwa safarini kwa kuelekea jijini Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, waliofunga barabara ili azungumze nao leo Septemba 29, 2015, wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.PICHA NA OTHMAN MICHUZI.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muheza wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Umati wa wakazi wa mji wa Muheza.
Ilikuwa ni furaha kwa kila aliemuona Mh. Lowassa alipokuwa akizungumza nao.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, mara baada ya kuzungumza nao, wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake leo Septemba 29, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia wananchi wa Mji wa Korogwe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga leo Septemba 29, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Korogwe, Mkoani Tanga, wakati wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga leo Septemba 29, 2015.

MAMA SAMIA SULUHU-MGOMBEA MWENZA ALIYEPANGA KUWAPIGANIA WANAWAKE

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM. Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM.

 MCHUANO wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajia kufanyika Oktoba 25, 2015 unaendelea maeneo mbalimbali ya nchini, huku vyama anuai vilivyofanikiwa kuingia katika ushindani huo wa kisiasa vikinadi ilani na sera zao kwa Watanzania ili kuwashawishi wachaguliwe.

 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mara ya kwanza kimemsimamisha mwanamke katika ngazi ya juu ya uongozi. Kimemteuwa mwanamama, Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza wa mgombea wa nafasi ya urais kupitia chama hicho, John Pombe Magufuli. 

Kwa mantiki hiyo endapo kitafanikiwa kushinda urais Tanzania kwa mara ya kwanza mwanamke atashika nafasi ya juu ya madaraka ndani ya Serikali. Bi. Suluhu ambaye amewahi kufanya kazi kama kiongozi katika Serikali zote mbili yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar (Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar-SMZ) anauzoevu wa kutosha na elimu nzuri inayomuongeze sifa ya kuimudu nafasi aliyopewa kwa sasa.

 Ki historia, Bi. Suluhu alizaliwa Januari 27, mwaka 1960 nchini na kupata elimu yake ya msingi na sekondari Zanzibar, kabla ya kuendelea na elimu ya juu kwa kozi mbalimbali katika vyuo vikuu vya Mzumbe nchini Tanzania, Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza kwa ushirikiano na Chuo Kikuu Huri cha Tanzania (OUT). [caption id="attachment_62370" align="aligncenter" width="741"]Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (kulia) akimjulia hali mmoja wa akinamama katika moja ya wodi za wazazi nchini. Kiongozi huyo anaahidi endapo atashinda uchaguzi kupitia chama chake ataziangalia zaidi huduma za afya ya uzazi ili kuboresha zaidi.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (kulia) akimjulia hali mmoja wa akinamama katika moja ya wodi za wazazi nchini. Kiongozi huyo anaahidi endapo atashinda uchaguzi kupitia chama chake ataziangalia zaidi huduma za afya ya uzazi ili kuboresha zaidi.

 Mwanamama huyu pia amefanikiwa kuchukua kozi ndogo ndogo anuai katika vyuo vya ndani na nje ya Tanzania, vikiwemo vya; 'Institute of Management for Leaders, Hyderabad, India', Zanzibar Institute of Financial Administration, ZIFA, pamoja na National Institute of Public Administration, Lahore Pakistan. Mgombea huyo mwanamama amekuwa waziri na mbunge kwa zaidi ya miaka mitano mfululizo na pia kufanikiwa kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, nafasi ambazo kwa kiasi kikubwa zinamuongezea sifa ya kuweza kuimudu nafasi aliyopewa kwa sasa anasema hii ni nafasi pekee kwa akinamama wote bila kujali itikadi zao kumuunga mkono ili aweze kushinda na kuweka historia nchini ya mwanamke kushika nafasi ya juu kuliko zote nchini. 

Kwa sasa kiongozi huyu anazunguka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani kuinadi ilani ya CCM. Bi. Suluhu anasema ilani ya CCM imepanga kufanya mengi mazuri kwa Watanzania, lakini pamoja na hayo amejitolea kuhakikisha anawapigania akinamama endapo atafanikiwa kushinda nafasi hiyo ili kuweza kukabiliana na changamoto anuai ambazo zimekuwa kero na kikwazo kwao.

 Anazitaja changamoto hizo ni pamoja na huduma za afya ya uzazi ambapo akinamama wengi na watoto wachanga wamekuwa wakipoteza maisha katika eneo hilo.

 Anasema licha ya ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kufafanua zaidi itakavyo boresha huduma za afya kiujumla, lakini atalisimamia na kuongeza nguvu za ziada kuhakikisha akinamama wanapata huduma za kuridhisha maeneo wanapopata huduma za afya ya uzazi. 

 Akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Jimbo la Mbulu Mjini anasema endapo CCM itashinda uchaguzi huu imepanga kuajiri watumishi 15,000 wa sekta ya afya wakiwemo madaktari 2020 ndani ya kipindi kifupi ili kuhakikisha inaboresha zaidi huduma za afya maeneo mbalimbali nchini hasa huduma za akinamama na watoto. 

Bi. Suluhu anasema hatua hiyo ni mpango maalumu wa kuboresha huduma za afya kiujumla na hasa huduma za akinamama wajawazito na watoto ambapo wamekuwa na changamoto katika huduma hizo.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akiinadi ilani mpya ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kwa wananchi (hawapo pichani) katika moja ya mikutano yake.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akiinadi ilani mpya ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kwa wananchi (hawapo pichani) katika moja ya mikutano yake.[/caption] Aidha anaongeza kuwa mpango mwingine ni kuwawezesha akinamama na vijana kiuchumi kupitia vikundi vyao.

 Anabainisha kuwa eneo hili Serikali ya CCM kupitia ilani yake imetenga shilimi milioni 50 kwa kila kijiji fedha ambazo zitakuwa zikikopeshwa makundi hayo kwa masharti nafuu ili waweze kujikwamua kiuchumi. Anasema eneo hilo pia halmashauri zitasimamiwa kutoa asilimia tano ya mapato kuwaunga mkono akinamama na vijana ili kuchochea maendeleo yao. 

Ili kukuza biashara zao Bi. Suluhu anasema Serikali itasimamia kuhakikisha asilimia 30 ya tenda ndogondogo za halmashauri mbalimbali zipewe vikundi vya akinamama na vijana.

 Anaeleza kuwa ili kuongeza thamani kwa mazao yatakaokuwa yakizalishwa na vikundi hivyo kupitia miradi ya kilimo imepanga kujenga viwanda vingi maeneo mbalimbali ya nchi ambavyo vitayaongezea thamani mazao na pia kuzalisha ajira kwa asilimia 40, jambo ambalo pia litakuza uchumia wa akinamama na vijana.

 Mwanamama huyo shupavu anabainisha kuwa kutokana na suala la kero ya maji pia kuwaumiza zaidi akinamama ilani ya chama chake imedhamiria kumalizia miradi ya maji na kuanzisha mingine anuai ili kukabiliana na changamoto ya kero ya maji safi na salama iliyopo maeneo mbalimbali ya nchini vijijini ama mjini.

 Bi. Suluhu anasema Serikali watakayoiunda itaendelea kushughulikia kero ya maji katika vijiji vyenye ukame na kuhakikisha kila kijiji kinapata maji safi na salama kwa matumizi. Lakini ili kumaliza kabisa kero hiyo anasema Serikali itaunda mfuko wa maji ambao utashughulikia kero za huduma za maji safi na salama. 

 Anasema migogoro yoyote inayosababisha mapigano idadi kuwa inayoathirika ni wanawake na watoto, hivyo Serikali itakayoundwa na CCM itahakikisha inapima ardhi yote ya vijiji pamoja na Wilaya na kuainisha mipaka ili kukomesha migogoro ya ardhi inayochangia mapigano ya wakulima na wafugaji baadhi ya maeneo ya Tanzania mara kwa mara.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (mwenye miwani) akisalimiana na baadhi ya akinamama na wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (mwenye miwani) akisalimiana na baadhi ya akinamama na wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM.

 Anasema mara baada ya kupima ardhi na kuweka mipaka kati ya maeneo ya wakulima na wafugaji watahakikisha mipaka hiyo inatambulika na kuheshimiwa na jamii zote mbili ili kuzuia migogoro na mapigano ambayo yamekuwa na uhasama mkubwa na kupoteza uhai na mali za raia wasio kuwa na hatia katika maeneo yenye mgogoro. 

 Hata hivyo katika kampeni zake mara zote amemalizia kwa kuwaomba wananchi kutunza amani iliyoasisiwa na viongozi wetu wa taifa kwa kutokubali kuyumbishwa na kushawishia kuvuruga amani ya nchi. "...Tusikubali kuchokozwa na kuchokoseka na kuvuruga amani...bila amani hakuna maendeleo," alisema Bi. Suluhu. 

 Anawataka viongozi wa siasa kuacha kutoa vitisho kwa wapiga kura kwani hali hiyo ni kuibaka demokrasia hivyo CCM na vijana wake hawatakuwa tayari kuona demokrasia inabakwa nchini na wapuuzi wachahe. "...Vijana wa CCM naomba mkikamata kibaka wa demokrasia shughulikeni naye kidogo kabla ya kumpeleka polisi...CCM itashinda kwa kishindo," alisema Nape Nnauye. Miongoni mwa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo kulingana na taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni pamoja na CCM, CUF, CHADEMA, UMD, NCCR- Mageuzi, NLD, UPDP, NRA, TADEA, TLP, UDP, DEMOKRASIA MAKINI, CHAUSTA, DP, APPT-Maendeleo, Jahazi Asilia, SAU, AFP, CCK, ADC, CHAUMMA na ACT-Wazalendo.
 *Imeandaliwa na www.thehabari.com

Monday, September 28, 2015

CHOPA YA CCM YATUA MANYARA,MWIGULU NCHEMBA AENDELEA KUKUSANYA KURA ZA CCM

Mwigulu Nchemba mmoja ya wajumbe 32 wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi akisalimiana na Wananchi wa Karatu Mjini jioni ya leo alipofika kwaajili ya Kuomba kura kwaajili ya Rais,Mbunge na Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi.
Sehemu ya Wananchi wa Karatu Mjini waliofika Uwanjawa Mazingira Bora kusikiliza Mkutano wa hadhara wa Mwigulu Nchemba.Mwigulu Nchemba akitoa darasa kwa Wananchi wa karatu kuhusu biashara ya Kumuacha Dr.slaa na kumpatia Edward Lowassa aliyehamia kutoka CCM.Dr.slaa aliyetumia Jasho na Damu kuuimarisha Upinzani wenye meno,Hii leo ameondolewa kwakuwa DILI imewekwa mezani ili Mtu mwenye kashafa mbalimbali chafu aweze kuwania Urais.Kwaaina ya Mgombea waliosimamisha UKAWA,Mwigulu amesema itakuwa rahisi sana kwa Magufuli kushinda kwa asilimia kubwa sana ya Kura.Wananchi wa Mbulu Vijijini wakisikiliza Mkutano wa Mwigulu Nchemba wakati akinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi.Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi wa BashinetMbulu Vijijini wakati alipokwenda kumuombea Kura Rais Mtarajiwa J.Pombe Magufuli na kuwanadi Madiwani na Wabunge wanaotoka Mkoa wa Manyara.Mwigulu Nchemba akiwasili Dongobesh kuzungumza na Wananchi kwenye Mkutano wa kampeni wa Chama cha Mapinduzi.Mwigulu NChemba akimnadi Mbunge mtarajiwa wa Jimbo Jipya la Mbulu Vijijini Ndg.Flatei hii leo wakati wa mkutano wa kampeni kata ya Dogobesh.Wananchi wa Dongobesh wakionesha ishara ya kuunga mkono Ilani ya CCM,Na kwamba wapotayari kumchagua Magufuli kwenye nafasi ya Urais,Flatei kwenye Ubunge na Madiwani wa CCM.Mwigulu Nchemba akiwasili Mbulu Mjini kwenda kuzungumz na Wananchi.Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa Mbulu Mjini hii leo,Amewaomba kuwa mabalozi kwa watu wote kuhusu Ubora wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi na Ubora wa Wagombea wa CCM kwa ngazi zote,"Kila mmoja ajitoe kuwa balozi wa kuhamasisha wananchi wanachagua CCM kwa ngazi zote kwakuwa CCM ndio chama chenye ilani bora na inayotekelezeka.Ndani ya Ilani ya CCM kunamaswala ya kimaendeleo hususani Ujenzi wa Barabara ya kutoka Bareda hadi Mbulu,Pia ujenzi wa Miundombinu ya maji."Mwigulu.
Hivyo wananchi wa Mbulu,Hakikisheni mnajitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura,na ichagueni CCM ikasimamie shughuli za maendeleo za jimbo la Mbulu Mjini na Vijijini.Wananchi wa Mbulu Mjini wakinyoosha mikono yao kuunga mkono ilani ya CCM na kuahidi kuichagua CCM kwenye Uchaguzi mkuu wa October 25.Kabla ya kufika Karatu Mjini,Mwigulu Nchemba alifanya mkutano kwenye kata ya mpakani mwa Mbulu Mjini na Vijijini.Katika mambo mengi anayozungumza Mwigulu Nchemba,Kubwa ameendelea kuwasihi Wananchi wafanye Uchaguzi wa Amani na Utulivu."Wananchi wa karatu,Kwanza nawapongezeni kwa ile hotuba ya Mzee wenu Dr.Slaa,Tunahitaji viongozi wanaosimama kwenye Maneno yao.Haiwezekani kwa miaka 20 wapinzani wamekuwa wakiimba kuwa Lowassa ni Fisadi,Lakini kwa sababu ya DILI,Siku moja wote wameamua kubaidlika na kumuunga mkono mtu aliyeliingiza Taifa hili kwenye Ufisadi mkubwa wa Richmond n.k.
Lakini kwa Dr.Slaa alionesha msimamo kama Mtanzania kuwa yeye si sehemu ya Ufisadi hivyo ataendelea kupinga Ufisadi ndio maana hakuwa tayari kumpokea Lowassa".
Mbali na hayo Mwigulu Nchemba ameendelea kuwasihi Watanzania kujitiokeza kupiga kura na Waichague CCM kwa maendeleo ya Karatu na Tanzania yote.Wananchi wa karatu Mjini wakifuatilia kwa Umakini Mkutano wa Mwigulu Nchemba.Mwigulu Nchemba aliwaasa watu wote wanaoamini katika Vurugu kuwa,Rais wa Tanzania atapatikana kwa kura kwenye sanduku la kupigia kura,Wanaolalamika kuwa wataibiwa kura ni wazi wanahofu kwasababu wameshashindwa kuanzia kusimamisha Mgombea hadi kwenye Uandaaji wa Ilani ya Uchaguzi.Kabla ya kuingia Mkoa wa Manyara,Mwigulu Nchemba mapema leo alizungumza na Wananchi wa kata ya Mitundu Jimbo la Manyoni Magharibi kuwaomba waichague CCM.
Picha na Sanga Festo Jr.