Tuesday, October 13, 2015

PINDI CHANA AMKABIDHI RAIS WA BARAZA KUU LA UN TAMKO LA KUTOKOMEZA NDOA ZA UTOTONI

 Mwenyekiti wa Mtandao wa Kimataifa wa Wabunge  (PGA) Mhe.  Pindi Chana ( MB) akimkabidhi Rais wa Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa,  Bw.Mogens Lykketoft,Tamko la  wabunge lenye sahihi 607 za wabunge kutoka mataifa 70 la  kutokomeza ndo za utotoni na za kulazimisha katika hafla fupi iliyofanyika  Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu.
 Mwakilishi wa Kudumu wa Zambia katika  Umoja wa Mataifa, Balozi Dr. Mwaba Kasese-Bota akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo alianisha mipango mbalimbali inayofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwamo viongozi wa kimila katika kuzunguia ndoa za utotoni na za kulazimishwa.
  Mwakilishi wa Kudumu wa Ghana katika Umoja wa Mataifa, Balozi Martha Anna Akyaa Pobea naye akitoa mchango wa namna  gani serikali yake inavyolishughulikiwa   tatizo za ndoa za utotoni ambapo amesema katika nchi za Afrika Magharibi katika kila watoto watano wa kike, wawili  huolewa kabla  ya kutimiza miaka 18 na kwamba ndoa hizo za utotoni si tu kwamba zinadumaza  ukuaji wake lakini pia zinachaniga mimba za umri mdogo,  vifo vitokanavyo na uzazi,  maambukizi ya magonjwa mbalimbali na kuchangia  umaskini kwa watoto wengi wa kike.
 Sehemu ya  washiriki wa hafla hiyo  wakiwamo  watalamu kutoka Wizara ya  Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wakiongozwa na  Kaimu Katibu Mkuu, Bi, Nuru Milao.

Na  Mwandishi Maalum, New  York
Mtandao wa Kimataifa  wa Wabunge kutoka  Mabunge mbalimbali  Duniani (PGA),  umemkabidhi Rais wa Baraza Kuu la  70 la Umoja wa Mataifa Bw. Mogens Lykketoft,  tamko   la kukomesha ndoa za utotoni  na za kulazimishwa kwa watoto wa kike.

Akikabidhi tamko hilo lenye sahini  Zaidi ya 607   kutoka nchi 70 Mwenyekiti  wa Mtandao huo wa wabunge,  Mhe. Pindi Chana na ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,  Jinsia na  Watoto amesema, kukabidhiwa kwa tamko  hilo kwa  Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  kunakwenda sambamba na  maadhimisho  ya siku ya mtoto wa kike ambayo   huadhamishwa  kila  Octoba ya mwaka.

Mwenyekiti wa  PGA, amesema wakati wa  hafla hiyo fupi iliyofanyika hapa  Umoja wa Mataifa, siku ya Jumatatu kwamba,  ushirikiano wa wadau mbalimbali hasa  wabunge , serikali na asasi za kiraia ni  muhimu sana ikiwa jumuiya ya kimataifa  inataka kuondokana na kumaliza tatizo la ndoa za utotoni na za kulazimishwa.

Mhe. Pindi Chana,  amesema, ni kwa kutambua ukweli huo ndiko kulikopelekea kuanzishwa kwa mtandao huo  mwezi Machi mwaka huu ambao moja na dhumuni lake kubwa ni kuwahamasisha, kuwaelimisha na kuwawezesha wabunge kutumia nafasi zao kukemea  tatizo hilo.

Hafla hiyo  iliandaliwa kwa  ubia kati ya Wakilishi za Kudumu za Tanzania, Zambia , Ghana na  Canada katika Umoja wa Mataifa. nchi ambazo  kwa namna moona ama nyingine zimekuwa  mstari wa mbele katika kuchangiza afya na maendeleo ya mtoto wa kike ili  mtoto huyo wa kike aweze kupata fursa  kukua, kuelimika     na hatimaye aweze kulitumikia taifa lake na watu wake katika ukamilifu wake.
Amebainisha  kwamba kama  viongozi, wabunge wanapashwa kuwahabarisha  wananchi wao, na wabunge wenzo thamani ya mtoto wa kike, na  umuhimu wa kuhakikisha kuwa mtoto wa kike anakwenda shule, anabaki shule na anamaliza masomo  yake.

“ Kama watunga sheria, wabunge tunapaswa kusimamia sheria zinazomlida mtoto wa kike ikiwa ni pamoja na kupitisha sheria zitakazo ainisha bayana umri wa kuolewa kwa mtoto wa kike ambao unapashwa kuwa miaka kumi na nane” amesititiza Mwenyekiti wa PGA.

Aidha  Mhe.Pinda Chana akaongeza pia kuwa wabunge na mabunge yanao wajibu wa kusimamia utekelezaji wa  Malengo ya Maendeleo Endelevu, na ugawaji wa  raslimali kwenye maeneo mpaya ya kisera na sera ambazo  tayari zipo.

 Akaongeza kuwa  Lengo namba 5.3 la maendeleo endelevu  linaainisha wazi wazi namna ya kushughulikia  vitendo  vinavyorudisha nyuma maendeleo na ustawi wa mtoto wa kike  katika  kile eneo, jambo analosema wabunge wanapashwa  kusimamia vema utekelezi wa  lengo hilo pamoja na mengine.

PAG inalenga pia kuwaelimisha wabunge  kutetea na kusimamia haki zinazomlinda mtoto wa kike,  kupiga vita mila na desturi  potofu zinazomkandamizi mtoto wa kike , kusimamia utawala wa sheria, demokrasia usawa wa binadamu, kupinga ubaguzi na kusimamia usawa wa kijinsia.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa  tamko hilo, Rais wa Baraza Kuu la  70 la Umoja wa Mataifa, Bw. Lykketoft amesema kuwa  tamko hilo limekuja wakati muafaka na hasa baada ya   Viongozi  Wakuu wa Nchi na Serikali  kupitisha kwa kauli moja  Malengo Mapya ya Maendeleo  Endelevu ( Agenda2030) mwezi  uliopita.

Akaongeza kuwa, akiwa Rais wa Baraza  Kuu la 70  atahakikisha kwamba nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa  zinaendelea na majadiliano  yenye tija na yakayolenga katika kuhakikisha utekelezaji wa Agenda 2030 na kutilia mkazo mijadala inayolenga katika mkomboa mtoto wa kike dhidi  ya  ndoa za utotoni na  za kulazimishwa.  Na pia  kuhakisha kwamba majadiliano  kuhusu mabadiliko ya tabia nchi yanafanyika kwa lengo la siyo tu kuiokoa  sayari dunia lakini pia maisha ya mwanadamu ambayo uhai wake unategemea sana uwepo wa sayari hiyo.

No comments:

Post a Comment